Na Hassan Mabuye

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ismani Mkoani Iringa kwa kushirikiana na Ubalozi wa Japan amesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa Mkoani Iringa kwa kiasi cha shilingi milioni 270.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Idodi Iringa Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida alisema kuwa misaada hiyo inatolewa kupitia kodi za watu wa Japan kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za kimaendeleo nchini Tanzania.

Ubalozi huo wa Japan ambao umesaidia ujenzi wa bweni la wanafunzi katika shule ya sekondari Idodi umetokana na maombi ya mbunge wa Jimbo hilo la Isimani Mhe. Wiliam Lukuvi aliyoyaomba katika ofisi ya ubalozi kufuatia bweni la awali la shule hiyo kuteketea kwa Moto.

Balozi huyo alisema kuwa mkataba wa ujenzi wa bweni hilo la wanafunzi Idodi sekondari ulisainiwa February mwaka 2016 kwa dolla za kimarekani 130,166 sawa na milioni 270 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi wa bweni hilo.

Ubalozi wa Japan nchini Tanzania umeahidi kuendelea kusaidia miradi mbali mbali ya kimaendeleo ndani ya mkoa wa Iringa na maeneno mengine hapa nchini ili kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli.
Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Bweni la wanafunzi wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bibi Amina Masenza.
Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida akiwa amevalishwa vazi la heshima la wazee wa kabila la Kihehe baada ya kuwezesha ujenzi wa Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto kwake ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
Balozi wa Japani nchi Tanzania, Masaharu Yoshida akiwa amevalishwa vazi la heshima la wazee wa kabila la Kihehe baada ya kuwezesha ujenzi wa Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa. Kushoto kwake ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliam Lukuvi na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi wilaya ya Iringa Mkoani Iringa.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa mbele.
Jengo la Bweni la Wasichana wa shule ya sekondari ya Idodi mkoani Iringa kwa nyuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...