Idara ya Uhamiaji inapenda kuutangazia umma kuwa imezindua rasmi huduma ya fomu ya maombi ya pasipoti mtandaoni (Online Passport Application Form). Huduma hii inapatikana katika tovuti ya Idara kupitia link ifuatayo: https://www.immigration.go.tz/ppt_application/ na itaanza kutumika rasmi kuanzia siku ya Jumatatu tarehe 07 Agosti, 2017. 

Kufuatia kuzinduliwa kwa huduma hii, waombaji wote wa pasipoti wanashauriwa kuzijaza fomu hizo mtandaoni, Kisha kuzichapisha (Printing) na kuziwasilisha katika Ofisi za Uhamiaji.

Hata hivyo, matumizi ya huduma hii yataenda sambamba na huduma inayotumiwa sasa ya fomu za maombi ya pasipoti mpaka pale itakapotangazwa vinginevyo. 

Utaratibu wa namna ya kujaza fomu hizo umeelekezwa katika fomu husika mtandaoni, na pia wateja wanaweza kupata ufafanuzi au maelezo zaidi kuhusu huduma hiyo kupitia anuani ya Idara ambayo ni  info@immigration.go.tz au katika Ofisi yoyote ya Uhamiaji iliyo karibu nao. 

Taarifa zaidi kuhusu huduma hii zitaendelea kutolewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
Imetolewa na:

KITENGO CHA UHUSIANO,
MAKAO MAKUU, IDARA YA UHAMIAJI,
04 AGOSTI, 2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...