JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kufanya misako, operesheni na doria zenye tija katika maeneo mbalimbali ili kudhibiti uhalifu na wahalifu na limekuwa likishirikiana na wananchi na wadau wengine katika jitihada hizo za kukabiliana na uhalifu na wahalifu na kupata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaongeza jitihada za kuzuia na kupunguza matukio ya ajali za moto kwa kuhakikisha wananchi wanachukua tahadhari dhidi ya matukio hayo. Aidha kumekuwa na ajali 01 ya moto kama ifuatavyo:-

Mnamo tarehe 15.08.2017 majira ya saa 21:30 usiku huko katika Soko la Sido Mwanjelwa lililopo Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jiji na Mkoa wa Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lilipokea taarifa ya kuwa Soko hilo lenye wafanyabiashara mbalimbali linaungua moto.

Kutokana na taarifa hizo, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama lilifika eneo la Soko la Sido ambalo lina wafanyabiashara mbalimbali wanaouza vitu mbalimbali na kuanza jitihada za kuzima moto pamoja na kuhakikisha usalama watu na mali zao.

Soko hilo limeteketea kwa moto na mali zote zilizokuwa katika soko hilo  ambavyo bado thamani yake haijafahamika. Moto huo ulizimwa majira ya saa 02:40 usiku wa kuamkia leo kutokana na jitihada za Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Kikosi cha zima moto na wananchi. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana. Hakuna mtu/watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo. Hakuna madhara ya kibinadamu yaliyoripotiwa kutokea.

Serikali kupitia Mkuu wa Wilaya ya Mbeya imeunda kamati maalum kwa ajili ya kufanya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo ikiwa ni pamoja na kujua chanzo cha moto huo pamoja na kufanya tathmini ya hasara iliyosababishwa na moto huo.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa pole kwa wafanyabiashara waliopoteza mali zao kutokana na janga hilo la moto na Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu. Pia tunatoa shukurani kwa wananchi kwa ushirikiano mkubwa uliosaidia kufanikisha kuzimwa moto huoili usilete madhara makubwa.

WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishina wa Polisi MOHAMMED R. MPINGA anatoa wito kwa wananchi kuepuka kukimbilia sehemu zenye majanga ya moto kwani ni hatari kwa maisha yao na badala yake wajenge tabia ya kutoa taarifa mapema taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuchukua hatua stahiki. Aidha katika matukio kama hayo wananchi wajiepushe na uporaji wa mali za watu badala yake wajikite katika uokoaji pekee.
 Imesainiwa na:
 [MOHAMMED R. MPINGA - DCP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...