Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (Mb), wapili kulia, akiwaongoza wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, kutembelea mradi wa umeme wa Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I jijini Dar es Salaam, Agosti 21, 2018. Kamati hiyo pia ilitembelea kituo cha kupkea gesi asili kilicho jirani na Miradi hiyo.


KAMATI ya Bunge ya Bajeti, imetembelea miradi ya kuzalisha umeme wa gesi ya Kinyerezi II, na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I unaoendeshwa na Serikali kupitia Shrika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi hiyo.

Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Mtwara vijijini Mhe. Hawa Ghasia, pia ilitembelea kituo cha kupokea gesi asili inayotumika kuzalisha umeme kilichoko jirani na miradi hiyo.

Katika ziara hiyo, mwenyeji wa Kamati hiyo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, (Mb), Mhe.Dkt.Medard Kalemani, aliwahakikishia wajumbe wa Kamati hiyo kuwa miradi hiyo inaendelea kama ambavyo Serikali ilitarajia na kwamba Watanzania wategemee ongezeko kubwa la upatikanaji wa umeme pindi miradi hiyo itakapokamilika. 
 Wajumbe wa Kamati wakipita pembezoni mwa moja ya mashine kubwa (genereta), kati ya 8 zinazofungwa kwenye mradi wa Kinyerezi II

“Mhe. Mwenyekiti na Wajumbe wote wa Kamati, miradi hii kunzia ule wa Kinyerezi I unaopanuliwa ambapo kutakuwa na ongezeko la umeme Megawati 35 na hivyo kufanya jumla ya Megawati 185 zitakazozalishwa kutoka Kinyerezi I, na huu wa Kinyerezi II utakapokamilika Agosti mwakani (2018) utatupatia Megawati 240 na ukijumlisha na miradi mingine itakayofuatia ya Kinyerezi III na VI, tutakuwa na jumla ya Megawati 1175.” Alifafanua Mhe. Dkt. Kalemani.

Kwa upande wake Meneja wa Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephene Manda aliwaambia wajumbe wa kamati hiyo kuwa mradi huo utakuwa na jumla ya mashine 8 ambazo zitafua umeme na tayari ufungaji wa mashine hizo umeanza na unaendelea na kuongeza kuwa kuanzia Desemba Mosi mwaka huu, TANESCO itaingiza megawati 30 kwenye gridi ya taifa na kufanya hivyo kila baada ya mwezi mmoja kadri kazi ya ufungaji wa mashine hizo utakavyokuwa unakamilika.

Alisema gharama za mradi wa Kinyerezi II ni dola milioni 344.

Mhandisi Manda, (waliyenyoosha mkono), ambaye ni Meneja Mradi wa Kinyerezi II, akwapatia maelezo wajumbe wa Kamati akiwemo Naibu Waziri Dkt. Kalemani. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...