Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewahimiza wakazi wa Kizimkazi kujiandikisha Bima ya Afya kwani ndio mfumo ambao utawawezesha kupata matibabu haraka na kwa gharama ndogo.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa Sherehe ya Siku ya Wakizimkazi ambapo siku hiyo wakazi hao hukutana na kupeana taarifa za maendeleo na kupanga mipango ya baadae kasha kula chakula cha asili pamoja na michezo ya asili.Mhe. Samia aliwaeleza wananchi hao kuwa hakutokuwa na mjomba atakayekuja kuwaletea maendeleo na alihimiza kwa kusema “Maendeleo ya Kizimkazi yataletwa na Wakizimkazi wenyewe”.

Katika Sherehe hizo Makamu wa Rais alifungua jengo la Ofisi ya Saccos ya Mkombozi lililopo Kizimkazi Dimbani na Kukagua maendeleo ya Ukumbi wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi.Mchezo wa Kuvuta ,kusokota kamba, kukuna nazi na mbio za Ngalawa zilionekana kuvutia watu wengi.

Makamu wa Rais alihimiza wanamichezo kujitokeza kwa wingi mwakani kwani michezo hudumisha umoja na kuleta mshikamano katika jamii.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jingo la Mkombozi Saccos lililpo Kizimkazi Dimbani wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkazi
Viongozi na Wageni mbali mbali walijumuika kula chakula cha asili cha Wakizimkazi wakati wa shrehe ya Siku ya Wakizimkazi.
Mashindano ya kukuna nazi yawa kizutio wakati wa Sherehe za Siku ya Wakizimkaziilaya ya Kusini mkoa wa Kusini, Unguja. 
Wananchi wakimpokea mshindi wa pili katika mashindano ya Ngalawa kijana Ahmed Yusufu Hassan ambaye ngalawa yake ameipa jina la Ndio Mambo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...