Na Mwamvua Mwinyi, Chalinze

MBUNGE wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amekabidhi pikipiki kumi, zilizogharimu sh. Mil. 22.5 kwa maafisa mifugo wa kata, ili waweze kuwafikia wafugaji wote, kupeleka sera ya kufuga kisasa na kuondoa migogoro na wakulima. Aidha amekemea tabia inayofanywa na baadhi ya wafugaji ya kufuga kizamani kwa kuswaga makundi ya ng’ombe kwenye eneo moja hali inayosababisha kuharibu rutuba.

Akikabidhi pikipiki hizo, huko Lugoba Ridhiwani alieleza, vyombo hivyo vya usafiri vikatumike kusimamia majukumu waliyonayo badala ya kuvitumia kwa matumizi yao binafsi. Aliwataka jamii ya wafugaji kuachana na mtazamo hasi wa kufuga kizamani mifugo lundo isiyo na tija pamoja na kuingia katika maeneo ambayo hayajatengwa kwa ajili yao.

Ridhiwani, alieleza kuwa wafugaji hasa wa kimasai wanaamini kuwa na ng’ombe wengi ndio utajiri, waondoe dhana hiyo kwani sio sifa, wajaribu kufuga mifugo michache na kujiwekea kasumba ya kufuga kwenye mazizi. Hata hivyo, alimpongeza mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze, Edes Lukoa kwa kusimamia na kuyafanyia kazi maazimio ya madiwani ambayo huwa wakitoa.

Ridhiwani, alito mafuta  lita tano kwa kila pikipiki na kuahidi kuangalia uwezekano wa kufanya utaratibu kila mwezi kwenye posho zinazokwenda katika kata maafisa mifugo hao wataongeza japo 5,000 kwa ajili ya mafuta ya pikipiki hizo.

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Lukoa alisema pikipiki hizo zimenunuliwa kutokana na mapato ya ndani ya halmashauri. Alizitaja kata zilizokabidhiwa usafiri huo kuwa ni sanjali na Vigwaza, Kibindu, Mbwewe, Talawanda, Msata, Kimange, Kiwangwa, Miono, Ubena Zomozi na Mandela.
Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akifurahi jambo na baadhi ya watendandaji wakati wa zoezi la kukabidhi pikipiki hizo.

Lukoa  alieleza kwa msimu wa bajeti 2017/2018 wanatarajia kununua pikipiki nyingine 15 kwa ajili ya watendaji na nyingine nane kwa ajili ya maafisa mifugo wa kata na vijiji. Aliwashukuru madiwani kwa ushirikiano na CMT kwa mchango  wao mkubwa katika kutoa maazimio yaliyotakiwa yatekelezwe na halmashauri na sasa yamefanikiwa. 

SOMA ZAIDI HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...