Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC umemalizika leo tarehe 20 Agosti 2017 katika mji wa Pretoria Afrika Kusini ambapo Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC kwa kauli moja wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake katika Asasi ya Ushirikiano wa siasa , Ulinzi na Usalama Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha uongozi wake akiwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo. 

Tanzania imemaliza kipindi chake cha Uenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama tarehe 19 Agosti, 2017 wakati wa Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa nchi wanachama wa SADC ambao umefanyikia hapa Pretoria, Afrika Kusini kuanzia tarehe 19 na 20 Agosti, 2017. 

Akizungumzia mambo muhimu yaliyojadiliwa katika mkutano huo wa 37 wa SADC, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema pamoja na mambo mengine SADC imetambua na kuthamini mchango wa Tanzania katika kipindi cha Uongozi wa Asasi ya Saisa , Ulinzi na Usalama iliyokuwa chini ya Rais Dkt. John Pombe magufuli. 
Makamau wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka saini moja ya makubaliano katika mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika wakati wa kuhitimishwa kwa mkutano huo mjini Pretoria. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
Dkt. Stergomena Tax akila kiapo mara baada ya kuteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa SADC .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais 
Makamau wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka saini moja ya makubaliano katika mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika wakati wa kuhitimishwa kwa mkutano huo mjini Pretoria. 
Dkt. Stergomena Tax mara baada ya kuteuliwa na kula kiapo kuwa Katibu Mtendaji wa SADC .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais 
.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...