Na Profesa Mark Mwandosya
Nimeona niandike waraka huu kutoka ughaibuni, ingawa si ugenini sana, nikiwa Jamhuri ya Comoro. Nimebahatika kusafiri sana kikazi duniani kote, kuanzia Japan mpaka Brazil, kuanzia Guyana mpaka Australia. Nimeiwakilisha nchi kikazi katika mabara yote isipokuwa Aktiki na Antaktika. 
Namshukuru Rabuka kwa kuniwezesha kulitumikia Taifa langu kwa zaidi ya miaka arobaini. Nimetembelea nchi zote jirani isipokuwa Jamhuri ya Comoro. Mara nyingi tumezoea kusema Tanzania inapakana na nchi nane; Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Watu ya Congo, Zambia, Malawi, na Msumbiji. Tunasahau kwamba watu wa Visiwa vya Comoro ni jirani zetu. 
Badala ya mpaka wa ardhi tunatenganishwa na Bahari ya Hindi. Inawezekana hii ikawa ndio sababu ya nchi zetu kutokuwa na ushirikiano wa karibu kiuchumi na kiutawala, pamoja na kwamba kijamii na kiutamaduni sisi, na hasa watu wa mwambao wa pwani na Zanzibar, Wacomoro wamekuwa ni sehemu yetu. Mara nyingi utasikia fulani na fulani wametutangulia mbele za haki na wamezikwa katika makaburi ya waComoro. 
 Nakiri kwamba pamoja na kusafiri sana nje ya nchi, sikuwahi kubahatika kufika nchi ya jirani ya Comoro. Hivyo basi nikiwa mstaafu, na ilhali Mwenyezi Mungu amenijalia siha njema, moja ya nchi ambazo nimeamua kutembelea ni nchi jirani, Comoro. 
 Nikiongozana na mke wangu Lucy, kijana wetu Emmanuel, tuliondoka Dar es Salaam kuelekea Moroni, mji mkuu wa Comoro, jumanne kwa njia ya anga kupitia ndege aina ya Bombadier, De Havilland Dash 200, Q400, ndege ya Shirika la ATC ambayo iliondoka kama ilivyopangwa, asubuhi saa 2 barabara. 
Muda mfupi baada ya ndege kufika usawa wa anga uliopangwa kwa safari hii, wahudumu wakatupatia, soda, kahawa au chai kwa jinsi kila msafiri alivyohitaji, vinywaji hivi vikiambatana na karanga na korosho. Hakika ndege ilijaa. Wasafiri wengi walikuwa ni wafanyabiashara wa Comoro wakitoka Dar es Salaam wakiwa na bidhaa mbali mbali. 
Hicho ni kielelezo cha jinsi ATC ilivyohodhi soko. Na kama itashindwa kuhudumia soko hili basi itakuwa ni kutokana na makosa yake na si vinginevyo.
Jengo la Abiria la Kiwanja cha Ndege cha Prince Said Ibrahim, Hahaya, Moroni 
Ofisini kwa Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Comoro
Msikiti wa Shiounda, Bangoi-Kouni, Ngazija.

Ndani ya Msikiti wa Shiounda, Bangoi-Kouni, Ngazija.

Mtaa wa Medina, Badjanani, Moroni, Ngazija.
Picha zote na Emmanuel Mwandosya.
Kupata chanzo na kusoma
 makala kamili BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...