Shamba la miti Sao Hill likishirikiana na Kampuni ya Art International limeanza utafiti wa kugema utomvu wa miti ya Misindano kama njia ya kujiongezea kipato kutokana utomvu huo kuuzwa kwa sh. 750 kwa kilo. 

Akizungumza na kamati ya Bunge ya Maliasili na Mabadiliko ya Tabia Nchi ya Malawi,Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill, Salehe Beleko  amesema katika kuongeza vyanzo vya Mapato wameingia mkataba na kampuni hiyo kufanya utafiti ni ikibainika kwamba haitaathiri Ukuaji wala Ubora wa miti wataidhinisha kuwa chanzo kipya cha mapato. 

Beleko amesema kwa kuwa ni utafitiwameanza kwanza na kwa miti iliyokuwa tayari kuvunwa wakiona hakuna Madhara wataendelea kwenye Miti michache yenye umri mdogo na matokeo ya utafiti huo yatapelekea ama kukuza ama kukataza kabisa zoezi hilo. 

Naye Mtaalam wa Kampuni ya China amesema Taasisi yake imefuata taratibu zote za ugemaji na usafirishaji wa utomvu huo na amefafanua kwamba kampuni yake inahitaji Miti Milioni 2 kwa mwaka ili kupata ujazo wa Utomvu wanaouhitaji. 

Akijibu swali la Mke wa Rais wa Zamani Bi Patricia Muluzi ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ambaye alitaka kujua matumizi ya Utomvu huo Mtaalam huyo amesema Baada ya kuchakatwa na kuchanganywa na kemikali mbalimbali utomvu huo hutumika kutengeneza dawa mbali mbali Bazoka (chewing gum), pamoja na Gel. 

 Rashid Pemba Msusa, mjumbe wa Kamati hiyo amesema kwa Mara ya kwanza wameshuhudia matumizi mapya kabisa ya zao la mti Teknolojia ambayo hawajawahi kuiona nchini kwao Malawi. Hata hivyo ameahidi kufuatilia matokeo ya utafiti huo ili ukifaa wauhamishie Malawi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...