Home
Unlabelled
TAJIRI ALIKO DANGOTE KUMTUMBUA KOCHA ARSENE WENGER ENDAPO ATAFANIKIWA KUINUNUA KLABU YA ARSENAL YA UINGEREZA
Mfanya biashara bilionea wa Nigeria Aliko Dangote amesema jambo la
kwanza atalofanya endapo atafanikiwa kuinunua klabu ya Arsenal ya Uingereza ni
kumtumbua kocha Arsene Wenger.
Toka
mwezi Mei mwaka 2015 Dangote amekuwa akikaririwa mara kwa mara kuwa ana mipango
ya kuinunua klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza ambayo mshika dau
mkuu wake ni bilionea wa Kimarekani Stan Kroenke anayeshikilia hisa asilimia 67
za klabu hiyo.
January
18 mwaka huu alipoulizwa, bilionea huyo namba moja wa Afrika alinukuliwa na
shirika la habari la CNBC akisema kwamba kwa sasa jicho lake kwanza liko kwenye
kuifanya kampuni yake ya Dangote Group kuwa na kiasi cha dola bilioni 100 kabla
ya kuinunua Arsenal.
"Nitainunua
(Arsenal) lakini kwanza nataka kuimarisha miradi yangu ambayo kwa sasa ni yenye
thamani ya dola bilioni 18, ndipo nitaigeukia Arsenal” CNBC ilimkarriri Dangote
wakati wa mkutano wa uchumi wa dunia huko Davos, Uswisi.
Dangote,
ambaye ni shabiki wa Arsenal na sio tena wa kocha Wenger, ameteka tena vichwa
vya habari karibuni kwa kusema jambo la kwanza atalofanya ni kubadili kocha.
“Amefanya kazi nzuri, lakini mtu mwingine inabidi aje kujaribu bahati yake”,
alisema alipohojiwa na Bloomberg.
Dangote
amekuwa mkosoaji mkubwa wa Wenger, akimshauri kocha huyo Mfaransa ‘kubadili
mfumo wake kidogo’ mnamo mwaka 2015. Lakini pamoja na kuonesha nia ya kuinunua
Arsenal, bado hajaweka dau mezani.
Yeye
anasema atafanya hivyo mara tu ujenzi wa mradi wake mkubwa wa mitambo ya
kuchakata mafuta wenye thamani ya dola bilioni 11 jijini Lagos utapokamilika.
Kampuni yake ya Dangote Group ilianzishwa mwaka 1977 ikiwa kampuni ndogo ya
biashara, lakini leo imekuwa kubwa na yenye matawi nchi kadhaa za Afrika
zikiwemo Tanzania, Benin, Ghana, Nigeria na Togo.
Hivi sasa
pamoja na kuzalisha saruji kampuni hiyo inazalisha pia sukari na vyakula.
Bilionea wa Kirusi Alisher Usmanov mwenye hisa asilimia 30 katika Arsenal
aliweka dau la dola 2.6 billioni ili kuinunua Arsenal mapema mwaka 2017 lakini
bilionea Kroenke mwenye hisa zaidi ya 67 aligoma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...