BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imeridhishwa na idadi kubwa ya watii
kutoka nchini China na kuelezea kuwa endapo kutakuwa na safari za
ndege za moja kwa moja kutoka Tanzania kutasaidia kupunguza gharama
za safari na pia kuchochea utalii.
Mwenyekiti wa Bodi ya TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo aliwaambia
waandishi wa habari jijini hapa juzi kuwa endapo kutakuwepo na ndege
ya moja kwa moja kutoka Tanzania mpaka China, idadi kubwa ya watilii
kutoka nchi hiyo itaongezeka na pia mataifa mengine, hivyo sekta ya
utalii uchangia zaidi mapato ya serikali.
akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kuwatembeza waandishi
waandamizi wa habari kutoka nchini China katika hifadhi za Ngorongoro
Crater na Manyara,Jaji Mihayo alisema vivutio vya utalii vilivyopo
hapa nchini ni tunu kubwa kwa taifa na pia vinawaleta watalii kutoka
sehemu mbalimbali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii(TTB) Bi.Devota Mdachi(wanne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja waandishi Waandamizi wa habari kutoka China walipotembelea hifadhi ya Ngorongoro Crater na Ziwa Manyara na kujionea fahari ya Tanzania. Lengo la ziara ya waandishi hao ni kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwenda kuvitangaza kupitia makala na machapisho ili kuvutia wachina wengi kutembelea Tanzania.
“Ujio wa wanahabari hawa ni fursa kwetu kwani watakwenda kuwa mabalozi
wazuri kwa kutoa machapisho na habari nchini kwao juu ya vivutio vya
utalii vilivyopo Tanzania,” alisema na kutoa wito kwa waandishi wa
ndani kuunga mkono jitihada hizo.
Alisema waandishi hao kutoka China wameonyesha nia ya dhati ya
kuvitangaza vivutio vyetu na hivyo kutokana na urafiki wa kihistoria
uliopo kati ya China na Tanzania, zoezi hilo litakuwa la mafanikio
makubwa.
Aliongezea kuwa China ni nchini yenye watu wengi Dunia hivyo kupitia
waandishi hawa watakwenda kuwafikia wananchi wengi wa nchi hiyo
kupitia makala na machapisho mbalimbali kuhusiana na vivutio vya
utalii vilivyopo Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.Jumanne Maghembe(kushoto) akizungumza na waandishi waandamizi wa habari kutoka China mara baada ya kumaliza ziara yao ya kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro Crater na Ziwa Manyara. Lengo la ziara ya waandishi hao ni kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kwenda kuvitangaza kupitia makala na machapisho ili kuvutia wachina wengi kutembelea Tanzania.
“changamoto kubwa waliyoiona ni gharama ya usafari wa ndege ni kubwa
kutokana na kutokuwepo kwa ndege za moja kwa moja,” alisema Jaji
Mihayo na kuongezea kuwa usafiri wa anga utakapo imarishwa utachochea
idadi kubwa ya watalii kutoka China.
Alisema tayari Rais Magufuli alishaahidi kuleta ndege Kubwa
itakayofanya safari ndefu hivyo itasaidia kupata soko la watalii
kutoka china kuongezeka na itasaidia kuongeza mapato katika sekta ya
utalii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...