Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa mwaka 2017.

Akiwasilisha Bungeni Muswada huo leo Mjini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa lengo la marekebisho yaliyopendekezwa ni kuboresha utekelezaji wa Sheria hizo kwa kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kutumia sheria hizo na kuongeza masharti mengine ili kuleta uwiano kati ya Sheria zilizorekebishwa na sheria zilizopo.

"Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa mwaka 2017 unapendekeza kufanya marekebisho katika sheria 11 na kufuta sheria moja" amefafanua Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 

Aidha, Masaju amesema kuwa masuala muhimu yaliyozingatiwa katika Muswada huo ni pamoja na kubadilisha vifungu vya Sheria kwa kufuta baadhi ya vifungu vya sheria hizo na kuviandika upya, kufuta baadhi ya maneno kwenye vifungu vya sheria, kuzingatia maneno mapya, kuongeza vifungu vipya na kufuta sheria moja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mohamed Mchengerwa amesema kuwa Kamati inashauri Serikali kuhakikisha Kamati maalumu ya kumshauri Waziri kuhusu misamaha ya kodi iundwe na wataalamu waliobobea kutoka katika fani na maeneo tofauti tofauti ili kujenga uwezo wa kamati hiyo katika kumshauri Waziri husika kuhusu misamaha hiyo ya kodi.

Nae Ally Saleh Ally kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Wizara ya Katiba na Sheria amesema kuwa kambi hiyo inashauri kuwa haitoshi kuifuta RUBADA pekee bali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu malalamiko ya wananchi wanaoituhumu kupora ardhi na hatua stahiki kwa wote waliohusika zichukuliwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...