Na Freddy Macha
Sarakasi ni kati ya sanaa hatari na za kusisimua sana.  Kwa sasa Ulaya wapo vijana na watu wa makamo mbalimbali waliohamia toka Afrika 

Mashariki (hasa Kenya na Tanzania) wakitumbuiza kadamnasi kwa sarakasi, Uingereza, Ureno,  Ujerumani na Hispania.
Nchini Hispania kuna visiwa vya Grand Canary ambapo Watanzania wachache hurukaruka kuvutia maelfu ya watalii.

 Moja yake ni Lanzarote. Hapa  Mtanzania Mohammed Idi Mohamed aliyehamia  baada ya kuishi Ujerumani kwa kipindi. Mohdy, Muddy au Modi (mwenye rasta fupi pichani) aliwahi pia kufanya kazi Tanzania, Ureno na Uingereza.
Alifariki Jumatatu 18 Septemba, 2017, asubuhi. Sababu za kifo chake zimeelezwa na waganga ni kuvuja damu kutoka mfereji wa koo kwenda mapafu na kutokea tumboni. 
Alipasukwa mshipa huu wa  damu ghafla na kuanguka bafuni akipiga mswaki. Bahati nzuri Muddy alijikatia bima ya maisha ambayo imeondoa tatizo la kusafirisha mwili wake nyumbani kuzikwa. Michango iiliyoombwa kutolewa itasaidia familia yake na gharama nyingine za mazishi.  Tuma kupitia Western Union. Huwa bei nafuu zikitumwa zifike kesho yake badala ya siku hiyo hiyo... Marehemu ameacha watoto wawili na wajukuu. Mungu aiweke roho yake pema peponi. 
Kwa walio Ujerumani, ni Malimbo Saidi Malimbo, simu (+49 ) 1522-4082848.
Uingereza, Saidi Kanda (+44) 4040-66607. Tanzania, Eddy Sengo,  (+255) 656 210 725.

Picha ihsani ya Fab Moses, Lanzarote, Hispania 
-London, 26  Septemba    2017

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...