Kupitia onyesho hili la Coke Studio linaloandaliwa na kampuni ya Coca Cola muziki wa Tanzania unazidi kutangazwa ikiwemo vipaji vya wanamuziki kutoka hapa nchini ambao wanashirikiana na wenzao kutoka Afrika na linarushwa kwenye luninga kwenye nchi zaidi ya 50 Onyesho la Coca Studio msimu huu barani Afrika linajumuisha wasanii kutoka katika nchi za Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Afrika Kusini, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar, Mauritius, Mozambique, DRC na Cameroon. Wasanii wa Tanzania waliopo katika onyesho la Coke Studio msimu huu ni Ali Kiba, Rayvanny, Izzo Bizness, na Nandy.

Wengine kutoka nchi nyingine ni Khaligraph Jones na Band Becca (Kenya),Sami Dan (Ethiopia),Bebe Cool, Eddy Kenzo, Sheebah, Ykee Benda ( Uganda). 

Wengine ni Nasty C, Busiswa, Mashayabhuqe kutoka Afrika ya Kusini, Youssoupha kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Runtown na Yemi kutoka Nigeria, Dji Tafinha kutoka Angola, Laura Beg kutoka Mauritius,Jah Prayzah na Slapdee kutoka Central Africa Republic, Bisa Kdei na Worlasi kutoka Ghana. 

Tangia onyesho hili lianzishwe limekuwa kiungo kikubwa cha kuwakutanisha wanamuziki wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na kupiga muziki wenye vionjo kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ikiwemo kuleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki.
Baada ya onyesho la pili la Coke studio msimu wa tano kupitia luninga ya Clouds kuacha gumzo kwa washabiki wengi wa muziki,mwishoni mwa wiki katika onyesho la tatu walipagaishwa tena na kolabo za wasanii mbalimbali zenye midundo ya kiafrika na zilizosukwa kwa ustadi mkubwa na magwiji wa kutengeneza muziki.

Wasanii waliotoa burudani kwenye onyesho la tatu ni mwanamuziki Nandy kutoka Tanzania ambaye amefanya kolabo na mwanamuziki Betty G kutoka Ethiopia ambapo wameimba kwa pamoja vibao vya Don’t break my heart na Mane Fistum, vilivyotengenezwa studio kwa umahiri mkubwa na mtengenezaji wa muziki nguli nchini Nahreel. Wasanii wengine ambao wamefanya kolabo ya kuvutia katika onyesho hilo ni Khaligraph Jones kutoka nchini Kenya akishirikiana na mwanamuziki Bruce Melodie kutoka nchini Rwanda. 

Kwenye onyesho la pili, Ali Kiba kutoka Tanzania, Patoranking kutoka Nigeria, Ozane kutoka Togo, Sami Dan kutoka Ethiopia, Laura Beg kutoka Mauritus, Sauti Sol kutoka Kenya na Chidinma kutoka Nigeria walionyesha umahiri wao katika tasnia ya muziki na kutawala jukwaa katika onyesho lao lililotengenezwa na nguli wa kutengeneza muziki wa studio barani Afrika kutoka nchini Nigeria, MasterCraft. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...