Na  Bashir  Yakub.

1.ZUIO  LA  MAHAKAMA  NININI.

Ni  amri  inayotolewa  na  mahakama  kumzuia  mtu  kutofanya  jambo  fulani  kwa  muda. Kampuni  nayo  ni  mtu  ambapo  yaweza  kuomba  zuio  au  kuzuiwa. Aidha yeyote  ana  haki ya  kuomba  amri  hii  ikiwa  anaona  kuna  jambo  fulani  linafanyika  na  ikiwa  litaendelea  kufanyika  basi  litaharibu  au  kupoteza  kabisa  kitu  fulani.

Kwahiyo  zuio   ni  amri inayobeba  maagizo  maalum  kwa  mtu  au  watu  maalum  kuwaamrisha  kutoendelea  na  kitu  fulani  kama  tulivyoona  hapo  juu.
Sheria  ya  Mwenendo  wa Madai,  Sura  ya  33 na  Sheria  nyingine  mtambuka  zimeongelea  kuhusu  zuio.

2.   KATIKA   MATUKIO   GANI  UNAWEZA  KUOMBA  ZUIO.

( a ) Kwa  mfano, umeshindwa  kulipa  mkopo  na  tayari  una  taarifa  kuwa  benki au  taasisi  yoyote  ya  fedha  inataka kwenda  kuuza  na  unahisi  kuna  pahala   hapaendi  sawa katika  mikataba yenu. Basi  unaomba  zuio  ili  hiyo  mali  yako  uliyoweka  rehani  isiuzwe  mpaka  hapo  hilo eneo  ambalo  mmeshindwa  kuelewana  litakapopatiwa  majibu.

( b ) Kwa mfano, umemuuzia  mtu  gari, pikipiki,  au  mashine  yoyote.  Mtu  huyo  hajalipa  kiasi  cha  pesa  iliyobaki kama  mlivyokubaliana. Lakini  anaendelea  kutumia  kifaa  hicho. Unaweza  kuomba   kumzuia  kuendelea  kutumia  mpaka  atakapolipa  kiasi  kilichobaki  ili  asiendelee  kuharibu  au  kuzeesha  kifaa  hicho.

( c ) Kwa  mfano, we  ni  mpangaji  katika nyumba ya kuishi  au  biashara.  Mwenye  nyumba,eneo anataka  kukutoa  kwenye  pango  hilo  bila  kufuata  utaratibu  au  kwa  kukiuka baadhi  ya  makubaliano  kwenye  mkataba  wenu. Unaweza  kuomba  zuio asiendelee  kukutoa.

Pia  mazingira  mengine  yoyote  ambayo  unahisi  kuna  kitu, jambo  linataka  kuharibiwa  au  kuingiliwa, kuuzwa, kupotezwa,kufichwa  kinyume  na  utaratibu  unaweza  kuomba  zuio  hilo.

KUSOMA   ZAIDI   sheriayakub.blogspot.com

                                        

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...