Na.Neema Mathias –MAELEZO.

Umoja wa wanawake wajasiriamali (MOWE) wameandaa tamasha la 11 kwa wajasiriamali litakalofanyika kuanzia tarehe 24-30 oktoba , 2017 katika viwanja wa mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam lengo ikiwa ni kupanua wigo wa masoko pamoja na kuonyesha bidhaa na fursa mbalimbali za kijasiriamali zinazopatikana hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati ya tamasha hilo, Bi. Zubeda Kiluwa amesema kuwa, tamasha hilo litakuwa na kauli mbiu isemayo‘Mwanamke mjasiriamali funguka shiriki kujenga Tanzania ya viwanda’

“Tunawaalika wanawake wote popote walipo kushiriki maadhimisho na maonyesho haya kwani yatawahusiha wadau mbalimbali wa maendeleo ya wanawake, Wizara pamoja na taasisi za serikali na mashirika binafsi,”alisema Kiluwa.

Tamasha hilo litafunguliwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwaijage ambapo wadau watakaoshiriki kutoa elimu za kijasiriamali katika tamasha hilo ni pamoja na Wakala wa Usajili Biashara na utoaji leseni (BRELA), TRA, GSM, SIDO, TBS, TFDA pamoja na wawakilishi kutoka katika benki mbalimbali ambao kupitia semina hiyo watatoa elimu juu ya ujasiriamali.

Aidha Bi.kiluwa ameleza kuwa gharama zitakazotozwa kwa wajasiriamali watakaoshiriki katika maadhimisho hayo ni shillingi 50,000 kila mmoja, na kwa yeyote atakayeshiriki kwaajili ya uzinduzi, ununuzi na kujionea bidhaa mbalimbali hawatatozwa gharama yoyote.

Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya tamasha hilo Bi.Anna Matinde amaesema kuwa tamasha hilo halitawahusisha wajasiriamali peke yake bali litawahusisha watu wote lengo likiwa ni kubadilishana mawazo ya kimaendeleo katika kuunga mkono sera ya Tanzania ya viwanda.

“Tanzania itajengwa na watu wengi, kupitiwa mawazo ya wajasiriamali na wale wasio wajasiriamali watapata kujua mambo mbalimbali juu ya elimu ya ujasiriamali, namna ya kujiajiri na kuondokana na wimbi la ukosefu wa ajira,” alifafanua Bi. Matinde.

Aidha Bi. Matinde amefafanua kuwa tamasha hilo halitowahusisha wanawake pekeyake bali hata wanaume wenye fursa mbalimbali za ujasiriamali wanakaribishwa kutangaza kazi zao na kujipatia elimu itakayotolewa .
Mwenyekiti na mjumne wa kamati ya maandalizi ya tamasha la 11 la Wanawake Wajasiriamali(MOWE) Bi.Anna Matinde akieleza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wajasiriamali Bi.Zubeda Lous na kushoto ni mjumbe wa Umoja huo wakati wa utambulisho wa tamasha na semina kubwa ya 11 litakalofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 24-30 oktoba ,2017 utambulisho huo ulifanyika hivi leo katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam.

Mjumbe wa Umoja wa Wanawake Wajasiriamali (MOWE) Bi.Zubeda Sembo akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kushoto ni Katibu wa Umoja huo Bi. Naomi Kamba na kutoka kulia ni mjumbe wa MOWE wakati wa utambulisho wa tamasha na semina kubwa ya 11 litakalofanyika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaa kuanzia tarehe 24-30 oktoba ,2017 utambulisho huo ulifanyika hivi leo katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam.
Picha na Paschal Dotto-MAELEZO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...