Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Wamiliki wa mitandao ya kijamii wameaswa kuchuja habari zao ambazo wamekuwa wakizipata na kuzisambaza kwa jamii kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa Redio ama televisheni za Mitandaoni.

Hayo ameyasema leo Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui , Valerie Msoka wakati alipokutana wamiliki wa mitandao ya Kijamii pamoja na waandishi wa habari, Valerie amesema kuwa upashanaji wa habari lazima kuangalia na usalama wa nchi pamoja kuacha uchochezi ambao unachonganisha na jamii au mamlaka.

Amesema kuwa takribani miaka mitano kulikuwa hakuna fursa za kupata matangazo ya televisheni kupitia mitandao ya kijamii, lakini sasa imeenea kwa watanzania wengi na inaendelea kuongezeka kadri ya teknolojia inavyokuwa, hivyo kunahitajika kuwepo umuhimu wa kusimamia huduma ya mitandao hiyo ili iweze kuleta tija kwenye taifa na si vinginevyo.

Valerie amesema kuwa TCRA kupitia kamati ya maudhui inatambua na kuthamini kuwepo kwa fursa ya upashanaji wa habari na serikali iliamua kuruhusu huduma hiyo wakati miongozo na taratibu stahiki zikiendelea kutayarishwa.
 
Amesema vyombo vya habari katika mitandao ya kijamii vya Radio, Televisheni na bado teknolojia inaendelea kukua na haviwezi kuzuia kutokana na mfumo wa upashanaji wa habari. Mwenyekiti huyo anasema habari zingine hazina tija kwa jamii na zingine zinaleta uchochezi ndani ya jamii na wakati mwingine kuingilia faragha za watu ambazo ambazo hazitakiwa kufikia jamii kama sehemu ya habari.

Amesema wadau wa mitandao ya kijami na watumiaji wa mitandao hiyo wanahakikisha wanahabarisha kwa kuzingatia habari zizojenga umoja wa kitaifa, mshikamano na ushirikiano baina ya watanzania bila kujenga hofu , kuchochea chuki na uhasama baina ya watanzania. Aidha amesema habari za matusi katika mitandao ya kijamii hayavumiliki ,kwani zinakiuka misingi ya uandishi na uhuru na wajibu wake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa TCRA, Valerie Msoka akizungumza na wadau wa mitandao ya kijamii juu uchujaji wa habari ambazo zinatakiwa  kuwafikia jamii na zinazolenga uimarishaji wa usalama wa nchi na mshikamano watanzania, leo jijini Dar es Salaam.Picha na Michuzi Jr-Michuzi Media Group.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa TCRA, Valerie Msoka (katikati) akipitia taarifa wakati wa mkutano wa wadau wa mitandao ya kijamii ambao wanasambaza taarifa leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maudhui, Abdul Ngalawa na Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka.
Kaimu Mkurugenzi wa Utangazaji wa TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka akizungumza katika mkutano wa wadau wa mitandao ya kijamii ambao wasambazaji wa taarifa kwa jamii leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya waandishi wa habari na wamiliki wa mitandao ya Kijamii wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.


Mmoja wa wamiliki wa Mitandoa ya Kijamii, kutoka Jamii Media Maxence  Mello akichangia jambo katika suala zima la uchujaji wa Habari katika mitandano ya Kijamii, katika mkutano uliowahusu Wamiliki wa radio, Televisheni za mtandaoni na mitandano mingine ya kijamii uliondaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),mapema leo jijini Dar
Mmoja wa wamiliki wa Mitandao ya Kijamii,kutoka Mtembezi Media,Antonio Nugaz akichangia jambo katika suala zima la uchujaji wa Habari katika mitandano ya Kijamii,ndani ya mkutano uliowahusu Wamiliki wa radio,Televisheni za mtandaoni na mitandano mingine ya kijamii uliondaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),mapema leo jijini  Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...