MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amezindua rasmi Ufyatuaji wa Matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za kisasa 402 za Walimu, ambapo amewaomba Wadau na Wananchi mbalimbali kuunga Mkono jitihada hizo.

Katika uzinduzi huo RC Makonda pamoja na kushiriki shughuli hiyo pia amebainisha kuwa la Ujenzi wa Ofisi hizo ni kuboresha Mazingira ya kufanya kazi kwa walimu ili waweze kutoa Elimu bora kwa Wanafunzi na kuongeza ufaulu.

Amesema wapo wengi waliopanga kufanya ujenzi wa Ofisi za Walimu lakini mipango hiyo iliishia kubaki kwenye makarabrasha maofisini lakini kupitia juhudi zake na Kamati aliyoiunda wameweza kuleta matokeo chanya.

RC Makonda ametoa wito kwa Wananchi na Wadau kuchangia Mabati, Saruji, Kokoto,Mchanga, Nondo au Nguvu kazi ilikuwawezesha walimu kufanyakazi katika mazingira bora.

Amesema ataki kuona kwenye Mkoa wake Walimu wanadhalilika kwa kukosa Ofisi na Vyoo hali inayopelekea kujisaidia kwa Majirani,Bar au Vichakani.

Aidha amesema hadi sasa amefanikiwa kupata mifuko zaidi ya 10,000 ya Saruji Mashine za kufyatulia Matofali,Gurdoza na vifaa vingine ambapo ataendelea kugonga hodi kwa Wadau ili waweze kuchangia ujenzi huo.

Amewaomba Wananchi kuwa na uzalendo kwa kujitoa katika ujenzi huo iwe kwa mtu binafsi au Vikundi vya Joaging,Timu za Mpira na vikundi vya maendeleo.

Ameipongeza Kamati ya ujenzi wa Ofisi za walimu,JKT,Jeshi la Magereza, Jeshi la Polisi,NHC, TBA,Channel Ten na Umoja wa Wamiliki wa Malori na wengine kwa namna wanavyojitoa kusaidia katika zoezi hilo.

Katika hatua nyingine RC Makonda amesema atatoa TV 30 kwa Magereza ya Ukonga, Segerea na Keko ili wafungwa wapate fursa za kutazama hotuba za Rais Dk. John Pombe Magufuli ili wajue maendeleo yanayofanyika uraiani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu Canal Charles Mbuge amesema hadi sasa kiasi cha fedha kilichotumika ni zaidi ya Million 200 ambapo watahakikisha ujenzi huo unakamilika.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizugumza leo katika uzinduzi wa Ufyatuaji wa Matofali kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za kisasa 402 za Shule katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akishiriki wa Ufyatuaji wa Matofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za kisasa 402  za Walimu, leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanel Massaka,Globu ya Jamii.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu Kanali Charles Mbuge akizungumza katika uzinduzi wa ufyatuaji tofali za ujenzi wa ofisi za shule katika mkoa wa Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...