Mwakilishi wa Benki ya Dunia (World Bank), Jonathan Marskell akizungumza kutambulisha wageni walioshiriki katika warsha ya wataalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano.
 Mhe. Balozi Hassan Yahya Simba akifungua warsa ya wataalamu wa wataalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano Bagamoyo.
Washiriki wa Warsha ya Teknolojia ya Mawasiliano Bagamoyo wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni Rasmi Mhe. Balozi Hassan Yahya Simba baada ya ufunguzi wa Rarsha.

WATAALAM wa Teknolojia ya Mawasiliano nchini wanakutana katika warsha ya Siku mbili mkoani Pwani kujadili namna ya kutengeneza mfumo wa Taifa wa Kidigitali utakaowezesha mifumo ya Serikali na Binafsi kubadilishana taarifa kwa kutumia Mfumo Mkuu wa Taifa wa Usajili na Utambuzi wa Watu unaosimamiwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA).

Warsha hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na World Bank na NIDA imefunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Balozi Hassan Yahya Simba ambaye amepongeza hatua hii muhimu kwa Taifa ya kuwa na mfumo utakaowezesha kuunganisha mifumo ya Serikali na Binafsi katika masuala ya Utambuzi kwa manufaa mapana ya Taifa.

Amesema kuwepo kwa mfumo imara wa Utambuzi kutawezesha sio tu maendeleo ya haraka ya Taifa, lakini pia kutaruhusu wananchi kupata haki zao kwa wakati na kuboresha huduma za kijamii; na kusaidia Serikali na sekta binafsi kuwafikia wananchi kirahisi  na kutoa huduma zenye viwango.

Akizungumza kwa niaba ya Benki ya Dunia (World Bank) ambao wamefadhili warsha hiyo, ndugu  Robert Palacios amesema Benki ya Dunia kwa kutambua umuhimu wa Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi na kwa kutambua changamoto kubwa ya idadi kubwa ya wananchi kutotambulika na mifumo rasmi kwa kukosa mfumo rasmi unaowatambua, Benki ya Dunia imeamua kusaidia harakati za nchi za Afrika katika kukamilisha kuanzishwa kwa mfumo wa Utambuzi na kuunganishwa kwa mifumo ya utoaji huduma ili kuwezesha wananchi kupata huduma kwa haraka na kuinua hali za maisha hususani wananchi wanaoshi katika hali ngumu.

Warsha ya Wataalamu wa Teknolojia ya Mawasiliano imeanza leo (18 – 19/09/2017) Bagamoyo mkoani Pwani katika hoteli ya Ocenic Bay na inatazamiwa kuibuka na maazimio yatakayoiwezesha Serikali kuwa na Sera na mikakati ya pamoja katika kuunda mfumo wa kidigitali wa matumizi ya Taarifa kwa Serikali na wadau katika utoaji huduma. Miongoni mwa washiriki katika warsha hiyo ni Wizara, Mashirika,  Taasisi na Makampuni binafsi. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...