Na Chalila Kibuda,
Globu ya Jamii
JUMUIYA ya Wazazi
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema wagombea ambao wataanza kampeni kabla ya
muda wajiandae kukatwa majina yao.
Akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Abdallah
Bulembo amesma kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinaendeshwa na kanuni hivyo
waombea wasipofuata kanunni hizo lazima wawe na roho ngumu pindi wanapokatwa
majina yao.
Amesema makatibu wa
Wilaya na Mikoa katika maeneo yao ikibainika kuwepo kwa rushwa katika uchaguzi
wa jumuiya hizo ajira zao ziko mashakani kuweza kuondolewa katika nafasi na
kuwapa watu wenye weledi.
Bulembo amesema
katika uchaguzi huo kwa ngazi ya taifa hagombei na kazi yake itakuwa kuwachuja
wagombea 49 waliogombea nafasi ya wenyekiti taifa.
Amesema katika
uongozi wake aliikuta akaunti ya jumuiya hiyo ikiwa na sifuri lakini sasa
akaunti hiyo ina fedha ambayo ataikabidhi baada ya uchaguzi huo
kufanyika.
Mwenyekiti huyo
amesema katika uongozi wake amepima viwanja 56000 vya jumuiya ya wazazi ,
uimarishaji wa shule ambazo zilikuwa zinaendeeshwa kama mali binafsi.
Bulembo amesema kuwa
katika mazoea ya uongzozi wake ni kutumikia kipindi kimoja ili aweze kukumbukwa
na watu waliomchagua.
Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Wazazi Taifa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) , Abdallah Bulembo (katikati)
akizungumza na waandishi habari juu ya uchaguzi wa jumuiya ya wazazi leo katika
makao makuu ya jumuiya hiyo leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Katibu Mkuu wa
Jumuiya hiyo Seif Shaaban Mohamed Bara na kulia ni Naibu Katibu Mkuu Jumuiya ya
Wazazi Bara, Barhan Abdul Ruta.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...