Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya Kituo cha Uwekezaji (TIC )na tovuti ya jijini Dar es Salaam.

Waziri wa viwanda Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage ameitaka bodi mpya ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania kushirikiana na menejiment ya TIC kuhakikisha uchumi wa viwanda unafanikiwa. 
Waziri Mwijage aliyasema hayo wakati akizindua Tovuti mpya na Bodi mpya ya Kituo cha Uwekezaji inayoongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Longinus Rutasitara ambaye ni msaidizi wa Raisi katika masuala ya uchumi.

Mh. Mwijage alisema “Mkakati wa Serikali ni kuendelea kukiwezesha Kituo chetu kuboresha  huduma chini ya “One Stop Facilitation Centre” kwani ni muhimu sana katika kuondoa usumbufu kwa wawekezaji na kujenga mazingira bora ya uwekezaji kwa wawekezaji wote walioamua kuwekeza hapa nchini.  Mwekezaji hana haja ya kuzunguka ili kupata vibali mbalimbali”. Hata hivyo waziri Mwijage aliasa taasisi zinazotoa huduma kupitia mahala pamoja yaani One Stop Centre chini ya TIC kuacha urasimu mara moja na kuomba TIC iweze kutoa taarifa mapema pale inapoona taasisi mojawapo inashindwa kutoa huduma kwa haraka na kuendekeza urasimu.

Naye Mwenyekiti mpya wa Bodi ya TIC Prof. Rutasitara amesema “Changamoto kubwa tunayoiona ni ile ya Kituo kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali katika kutafuta maeneo yenye ardhi yanayofaa kwa ajili ya uwekezaji. Bodi yangu itahakikisha kuwa inashauri ipasavyo kuhakikisha Kituo kinatengeneza na kuandaa ardhi ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji mkubwa. Katika kufanikisha hili, Bodi inashauri Kituo kibuni mbinu za upatikanaji wa ardhi ili kuondoa uwezekano wa Kituo au Mwekezaji kuingia katika migogoro ya ardhi hapa nchini”.

Akimshukuru Waziri wa Viwanda, biashara na Uwekezaji kwa kuchagua bodi makini kwa TIC, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Ndg. Geoffrey Mwambe amesema “Kituo kimeweza kuanzisha Kamati Maalum ya Kitaifa ya Kuhudumia wawekezaji yaani National Investment Facilitation Committee ambapo matokeo makubwa yameweza kuonekana kutokana na uboreshwaji wa huduma zetu za pamoja one stop facilitation centre”.

Aliongeza kuwa uzindunzi wa tovuti mpya ya TIC www.tic.go.tz ni  ishara kubwa kuwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania kimedhamiria kutangaza fursa za uwekezaji nchini ili wawekezaji waweze kuzifahamu na kuwekeza. Amesema kuwa tovuti hii mpya itakuwa chachu katika utoaji wa taarifa mbalimbali zihusuzo fursa na huduma mbalimbali za uwekezaji na mazingira ya uwekezaji hapa nchini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji (TIC), Profesa Longinus Rutasitara akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya na tovuti ya TIC jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Geoffrey Idelphonce akizungumza katika uzinduzi wa Bodi ya wakurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...