Na Teresia Mhagama, DSM.

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani na Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Mohamed Al Rumhi wamekutana  jijini Dar es Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano lengo likiwa ni kuendeleza Sekta ya Nishati nchini.

Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za Wizara jijini Dar es Salaam ambapo Waziri huyo kutoka Oman aliambatana na Waziri wa Uwekezaji na Biashara ya Nje wa Oman, Naibu Waziri wa Utalii na Balozi wa Oman nchini Tanzania.
Kwa upande wa Tanzania, viongozi mbalimbali walishiriki katika majadiliano hayo akiwemo Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Naibu Katibu Mkuu, Dkt Mhandisi Juliana Pallangyo na watendaji wengine kutoka Idara ya Nishati na Sheria.

Kwa upande wake Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Rumhi, alisema kuwa lengo la Ujumbe huo kufika wizarani ni kujadiliana na watendaji wa Wizara ya Nishati kuhusu maeneo ambayo ingependa ishirikiane na nchi hiyo ya Oman na kwamba nchi hiyo ipo tayari kushirikiana  na Tanzania.

“ Hapo zamani, Sisi Oman hatukutumia Gesi yetu vizuri kwa kuwa tulifanya haraka kuiuza nje ya nchi lakini ninyi mnayo fursa sasa ya kuitumia gesi yenu ndani ya nchi ili kutengeneza ajira pamoja na kuiendeleza kwa matumizi mbalimbali, na ikiwa ziko fursa za ushirikiano ili kuendeleza nishati hii, sisi tupo tayari,” alisema Dkt. Rumhi.
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Tano kulia),  Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Mohamed Al Rumhi (wa Nne kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Uwekezaji na Biashara ya Nje wa Oman, Dkt. Salim Al Ismaily (wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Maitha Al Mahrouqi, (wa pili kushoto), Balozi Mteule wa Oman hapa nchini, Ali Al Mahruqi (wa kwanza kushoto), Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa nne kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa Tatu kulia), Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kulia) na Balozi wa Tanzania nchini  Oman, Abdallah Kilima, (wa pili kulia).
 Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa nne kushoto),  Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Mohamed Al Rumhi (wa Nne kulia) wakiwa katika Ofisi ya  Waziri wa Nishati jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Uwekezaji na Biashara ya Nje wa Oman, Dkt. Salim Al Ismaily (wa tatu kulia), Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Maitha Al Mahrouqi, (wa pili kulia), Balozi Mteule wa Oman hapa nchini, Ali Al Mahruqi (wa kwanza kulia). Wengine ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa tatu kushoto), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa pili kushoto), na Balozi wa Tanzania nchini  Oman, Abdallah Kilima, (wa kwanza kushoto).
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (wa Tano kulia),  Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Dkt. Mohamed Al Rumhi (wa Tatu kushoto)  wakiagana mara baada ya kikao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Uwekezaji na Biashara ya Nje wa Oman, Dkt. Salim Al Ismaily (wa pili kushoto), Naibu Waziri wa Utalii wa Oman, Maitha Al Mahrouqi, (wa kwanza kushoto),  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (wa nne kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Wizara, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (wa Tatu kulia), Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kulia) na Balozi wa Tanzania nchini  Oman, Abdallah Kilima, (wa pili kulia).

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...