Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema kuwa  Jeshi hilo litaendelea kuwakamata na kuwachukulia hatua watu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu pamoja na wanaojihusisha kuwafadhili wahalifu kutekeleza uhalifu
IGP Sirro amesema hayo akiwa Ikiwiriri mkoani Pwani kwa lengo la kuzungumza na wazee pamoja na viongozi wa kidini wa wilaya zote mbili za Kibiti na Ikwiriri, kutokana na ushirikiano walioupatia Jeshi hilo wakati wa kukabiliana na vitendo vya mauaji vilivyokuwa vikitekelezwa na watu wasiowaadilifu.
Aidha IGP Sirro amelipongeza Jeshi hilo kwa Operesheni zinazoendelea nchini hususan katika mkoa wa Mtwara, zilizofanikisha kukamatwa kwa milipuko 16, visu 97 pamoja na mbolea ya chumvi inayotumika kuchanganyia kutengeneza milipuko pamoja na watuhumiwa kadhaa.
Kwa upande wake Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi Liberatus Sabas, amesema katika operesheni zilizofanyika mkoani Mtwara, wamefanikiwa kuwakamata watu kadhaa wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu na kwamba operesheni kama hizo bado zinaendelea.
Akiwa mkoani Pwani, IGP Sirro, pia amewapandisha vyeo jumla ya askari 43 kutokana na kufanya kazi kwa kiwango cha juu huku akiwataka kuendelea kufanykazi zao kwa weledi katika kuwahudumia wananchi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akimsalimiana na viongozi waandamizi na maofisa wa Jeshi hilo alipowasili Ikwiriri Mkoani Pwani kwa lengo la kuzungumza na wazee na wananchi wa Wilaya zote mbili za Ikwiriri na Kibiti.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiteta jambo na Mkuu wa operesheni maalum za Jeshi hilo, DCP Liberatus Sabas alipowasili Ikwiriri mkoani Pwani kwa lengo la kuzungumza na wazee na wananchi wa Wilayay zote mbili za Ikwiriri na Kibiti. Kulia ni Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai, DCI Robert Boaz.
Baadhi ya milipuko 16, Visu 96 na mbolea ya chumvi inayotumika katika kuchanganyia milipuko ikiwa imekamatwa Mkoa wa Mtwara kufuatia operesheni zinazoendelea za jeshi la Polisi. Picha na Jeshi la Polisi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...