Mamlaka ya mapato nchini (TRA) iliendesha na kudhamini shindano la shule za sekondari za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani jijini humo. Mashindano hayo yaliyoshirikisha shule mbalimbali za Dar es salaam na Pwani lilipambwa na maigizo ya maswala ya kodi ambapo mgeni Rasmi alikuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere.

Shule ya Sekodari Misitu iliyotia fora katika ufunguzi wa mashindano hayo ulimvutia mgeni rasmi na kudhamiria kushiriki mashindano hayo mwanzo hadi mwisho ambapo alipata fursa ya kujionea na kufurahia vipaji vya wanafunzi waliondaliwa vyema kuwa mabalozi wa maswala ya kodi katika nyanja mbalimbali kwa sasa na siku zijazo. 

Baada ya kufungua mashindano hayo yaliyonogeshwa na wanafunzi wenye vipaji mbalimbali vya kuwasilisha mada hatimaye shule ya sekondari Tumbi iliibuka kidedea na kujinyakulia zawadi mbalimbali ikiwemo Kombe, Luninga ya Kisasa, Saa ya Ukutani pamoja na cheti. 

Shule ya Sekondari Minaki ilichukuwa nafasi ya pili ikijinyakulia pia Kikombe, Komputa, Printa, Saa ya ukutani na cheti huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Shule ya Sekondari Maarifa ambayo kadhalika ilipata Kikombe, Komputa, Saa ya Ukutani pamoja na cheti.

Hadija Jumanne Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Misitu aliibuka Muwasilishaji mada bora na kujinyakulia Komputa mpakato, Saa ya Ukutani, Kikombe cha chai chenye chapa ya TRA. 

Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere baada ya kukunwa na uzuri wa mashindano hayo aliahidi kuyaboresha zaidi mwakani ili kuwapa motisha zaidi wanafunzi na walimu wao kujiandaa vyema na kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa kodi ambayo ndio mhimili muhimu wa kuboresha huduma za jamii na kuleta maendeleo kwa nchi. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) akiwasili ukumbi wa Chuo cha Kodi (ITA) kuhudhuria mashindano ya Kodi kwa Shule za Sekondari za Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani yaliyoendeshwa na kudhaminiwa na mamlaka hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kutoka (kulia) ni Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Philip Mbati na Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo. Kamishna huyo aliyekuwa mgeni rasmi alihudhuria shindano hilo mwanzo hadi mwisho. 
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) akimkabidhi Hadija Jumanne Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Misitu baada ya kuibuka mwanafuzi bora katika uwasilishaji wa mada ihusuyo kodi ya ongezeko la thamani (VAT), wakati wa shindano la maswali ya Kodi lililoendeshwa na kudhaminiwa na mamlaka hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kamishna huyo aliyekuwa mgeni rasmi alihudhuria shindano hilo mwanzo hadi mwisho. Pamoja naye (kulia) ni Mwakilishi wa Kamishna wa idara ya walipakodi wakubwa, Yeremiah Mbaghi na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Philip Mbati. (Imeandaliwa na Robert Okanda Blogs).

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere (wa pili kulia) akimkabidhi Mwalimu shule ya Sekodanri Jangwani zawadi ya kikombe baada wakati wa shindano la maswali ya Kodi lililoendeshwa na kudhaminiwa na mamlaka hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kamishna huyo aliyekuwa mgeni rasmi alihudhuria shindano hilo mwanzo hadi mwisho. Pamoja naye (kulia) ni Mwakilishi wa Kamishna wa idara ya walipakodi wakubwa, Yeremiah Mbaghi, Mkurugenzi wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo (wa tatu kulia) na Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA), Philip Mbati. 
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee wakiwa wamembeba mwalimu wao Boniface Mulambo baada yakukadidhiwa zawadi ya Kikombe na Kamishna Mkuu wa TRA, Charles Kichere kwa kuwaandaa vyema wanafunzi wake walioshiriki mashindano hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...