Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula na Mbunge wa Ilemela, ameishukuru Kampuni ya GF Trucks & Equipments kwa kutimiza ahadi yao kwa Mbao kwa kukabidhi gari yenye thamani ya milioni 70 na tayari wakiwa wamelipia gharama zote za ushuru na kufikia jumla ya milioni 100. 

Mabula amesema kuwa baada ya kuingia mkataba na kampuni hiyo wameanzisha kampeni ya ubingwa ili kulitoa taji kwa timu za Mkoa wa Dar es Salaam na wanaweza kufanikiwa kwa hilo kama wadhamini watajitokeza kwa wingi kwa timu za mikoani.

Mbao FC ya Mwanza imekabidhiwa basi lenye thamani ya Sh70 milioni kwa ajili ya wachezaji.Basi hilo wamekabidhiwa leo Jumatano na wadhamini wao Kampuni ya GF Trucks & Equipments katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Vingunguti, Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya GF Trucks & Equipments Alijawad Karmali alisema basi hilo ni sehemu ya mkataba ambao waliingia na Mbao miezi miwili iliyopita na wameweza kutimiza ahadi hiyo na wanaimani kuwa watalitunza katika kipinci chote..

Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Njashi amewashukuru Kampuni ya GF Trucks & Equipments kwa udhamini huo mkubwa waliouweka kwani mpaka basi hilo wanalipokea katika mikono yao limezidi thamani ya Sh70 milioni na litakuwa msaada mkubwa sana kwa timu yao kuhusiana na masuala ya usafiri na pia mpaka sasa udhamini wao umeshazidi milioni 140 

Mbao inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi sita, huku Simba ikiwa kileleni na pointi 12 ikifuatiwa na Yanga ambayo ndiyo mabingwa watetezi wakiwa na tofauti na mabao ya kufunga na kufungwa.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula akiwashukuru kampuni ya FT Trucks & Equipments kwa kuipatia udhamini kwa timu ya mkoani kwake Mwanza pamoja na basi sambamba na yeye kuwa mlezi wa timu hiyo leo Jijini Dar es salaam.
Ofisa Masoko wa Kampuni ya GF Trucks Equipment, Kulwa Bundala akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuwakabidhi gari lenye thamani ya milioni 70 kwa timu ya Mbao ikiwa ni moja ya makubaliano yaliyopo katika udhamini wao wa mwaka mmoja kwa timu hiyo. 
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula pamoja na Mkurugenzi wa GF Trucks & Equipments Alijawad Karmal (kulia) na mwenyekiti wa timu ya Mbao Solly Zephania Njashi wakikata keki.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maendeleo na Makazi Angelina Mabula akikata utepe katika gari ya waliokabidhiwa Mbao na kampuni ya GF Trucks & Equipments lenye thamani ya milioni 70 ikiwa ni katika makubaliano ya mkataba walioingia miezi mitatu iliyopita, juu ni Mkurugenzi wa GF Trucks & Equipmens Alijawad Karmal akimkabidhi mfano wa funguo ya gari mwenyekiti wa timu ya Mbao Solly Zephania Njashi akishuhudiwa na viongozi wengine wa Mbao Fc pamoja na wengine kutoka GF Trucks & Equipments.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...