NEC-DODOMA

Tume ya Taifa ya uchaguzi imesisitiza kuwa Leseni za udereva, Hati za Kusafiria na Vitambulisho vya Taifa vitatumika kwenye uchaguzi mdogo wa Madiwani wa Kata 43, utakaofanyika Novemba 26 mwaka huu.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Ramadhan Kailima amesema wapiga kura wataruhusiwa kutumia vitambulisho hivyo kwa sharti ya kwamba picha, herufi na majina yaliyopo kwenye Leseni ya Udereva, Hati ya kusafiria na Kitambulisho cha Taifa yawe yanafana na majina na herufi zilizopo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Kailima amesema kuwa ruhusa hiyo ya Tume ya matumizi ya vitambulisho hivyo imekuja kufuatia maoni ya wadau na baadhi ya wapiga Kura kupoteza kadi zao za kupigia Kura na wengine kadi zao kuharibika kutokana na sababu mbalimbali na hivyo kuwanyima haki na fursa ya kupiga Kura katika uchaguzi huo mdogo.

Amesema hatua hiyo inazingatia matakwa ya Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kifungu Namba 61, kifungu kidogo cha 3a na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kifungu Namba 62 (a) ambavyo vinaipa Tume mamlaka ya kuruhusu kutumika kwa utambulisho mwingine wowote utakao msaidia mpiga kura aliyejiandikisha kuweza kupiga kura iwapo hana kadi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...