Katika jitihada za kukabiliana na kuhimili athari za mabadiliko ya Tabianchi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kutafuta fedha kwa wafadhili na wadau wa maendeleo ili kupambana na changamoto hii inayoikabili dunia kwasasa.

Waziri January Makamba ameyasema hayo mara baada ya kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa ukuta wa kuhimili wingi wa maji na upandaji wa mikoko katika eneo la Kilimani na Kisakasaka Unguja.

Athari za mabadiliko ya tabianchi ni dhahiri kwa sasa, sisi kama serikali tunachukua hatua za dhati ikiwa ni pamoja na kutafuta fedha sehemu mbalimbali duniani ili kuendelea kutekeza miradi mingi zaidi kama hii ya kupanda mikoko na kujenga kuta zitakazosaidia kupunguza kasi ya maji kufika kwenye makazi ya watu, Makamba alisisitiza.

Waziri Makamba ameainisha kuwa lengo la Serikali ni kulinda na kuokoa uchumi wa wananchi wa kuweka miundombinu wezeshi kwa ustawi wa maendeleo endelevu. "ingawa masuala ya mazingira si jambo la muungano lakini hatuna budi kusaidiana na kushirikiana" alisema Waziri Makamba.

Nae msimamizi wa mradi huo Mhandisi Khamis Nassoro kutoka Kampuni ya Dezo Civili Contractors amesema kuwa changamoto kubwa ni uelewa mdogo wa wananchi juu ya hifadhi ya mazingira na kuwata wananchi wote kufahamu kuwa suala la kutunza na kuhifadhi mazingira sijukumu la serikali bali ni wajibu wa kila mmoja wetu.

Mradi huo unatekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia mazingira unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi minne na utagharimu dola za kimarekani 74,166.02
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akikagua eneo lililopandwa miti aina ya mikoko katika eneo la Kisakasaka Unguja. Azma ya Serikalini kuhakikisha maendeleo endelelevu kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Kulia ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mazingira Bw. Sheha Mjaja.
Pichani ni miti aina ya mikoko iliyopandwa katika eneo la Kilimani - Unguja ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Fedha za kupanda mikoko hiyo ziko chini ya mradi wa Kuhimili mabadiliko ya tabianchi unasimamiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...