Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imetoka sare ya 1-1 na timu ya Taifa ya Malawi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika leo katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ulioanza kwa kasi kwa kila upande uliweza kudumu kwa dakika 40 kwa timu ya Malawi kupata goli la kuongoza likifungwa na Robert Ng'ambi.

Goli hilo liliweza kudumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha Pili kilianza kwa Tanzania kutafuta goli la kusawazisha ambapo dakika ya 57, Simon Msuva akiisawazishia Tanzania goli na kupelekea matokeo kuwa 1-1.

Mpira ulianza kuwa wa vurugu baada ya Kocha wa Malawi kutolewa nje Na mwamuzi Israel Nkongo ikiwa ni kwa kufanya kosa la kuingia ndani ya uwanja na kubishana na mwamuzi wa akiba.

Ikiwa ni katika kutafuta goli la ushindi Beki wa kulia Erasto Nyoni aliweza kuzawadiwa kadi nyekundu na kisha baadae Mzamiru Yassin nae aliweza kupewa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.

Mpaka mpira unamalizika Taifa Stars 1- 1 Malawi.
Nahodha wa timu ya Taifa, Mbwana Samatta akiondoka na mpira mbele ya Mabeki wa Malawi.


Mmoja wa Wachezaji wa timu ya Tanzania (Taifa Stars) akimchomoko mchezaji wa timu ya Taifa ya Zambia,ambapo mpaka sasa kipindi cha pili timu hizo zimefungana sare ya 1-1 na mpira unaendelea katika uwanja wa Uhuru,jijini Dar.
 Kikosi cha timu ya Taifa Stars
 Waziri wa Habari,Utamaduni ,sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe akiikagua timu ya Taifa Stars kabla ya mchezo wa kirafiki wa Kimataifa dhidi ya timu ya Malawi kuanza jioni ya leo katika uwanja wa Uhuru,jijini Dar
 Wimbo wa Taifa Ukipigwa
Kikosi cha timu ya Malawi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...