Na Fredy Mgunda,Iringa

Wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wametoa msaada wa mashuka sabini na tano na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 1,672,500 katika hospitali ya Tosamaganga iliyopo katika katta ya kalenga mkoani Iringa kwa lengo la kuendelea kuboresha sekta ya afya ikizingatiwa kuwa wengi wao waliwahi kutibiwa hapo wakati wanasoma.

akizungumza wakati wa hafla ya kukadhi msaada huo mwenyekiti wa kamati ya Tosamaganga Alumni association ambaye pia ni mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Umoja Switch inayotoa huduma ya mashine za kutolea fedha (ATM) katika benki mbalimbali nchini, Danford Mbilinyi alisema kuwa walijipanga kuja kutoa msaada huu kwa kuwa wangi wao walikuwa wanatibiwa katika hospital hiyo wakati wakiwa masomoni miaka mingi iliyopita.

“Leo hii tunaafya njema kwa ajili tulitibiwa vizuri kipindi tulivyokuwa tunaumwa na ilitusaidia kufanya vizuri masomo yetu na ndio maana leo hii tupo hapa bila kupata huduma iliyobora nafikiri wengi wetu tusinge kuwa hapa” alisema Mbilinyi

Mbilinyi alisema kuwa wamechangisha kidogo walichopata wameamua kununua vifaa hivyo ambavyo wanafikiri vitakuwa na msaada kwa wagonjwa waliopo hospitalini hapo.

“Hiki kidogo tu lakini tunajua kwa namna moja au nyingine vinaweza kuwasaidia wagonjwa na kuwapunguzia mzigo uongozi wa hospitali yetu pendwa ambayo imekuwa ikitutibu kwa muda mrefu sana kipindi tukiwa masomoni katika sekondari ya Tosamaganga” alisema Mbilinyi.
Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wakiwa wanajadili kitu walipokuwa kwenye ziara ya kuitembelea shule waliyosoma
Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wakiwatembelea wagonjwa katika hospitali ya Tosamaganga mkoani Iringa
Baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma shule ya sekondari ya Tosamaganga iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa maarufu kwa jina la Tosamaganga Alumni Association wakiwa katika hospital ya Tosamaganga.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...