Na Globu ya Jamii, Dar es Salaam

Wanawake wametakiwa  kujitokeza kwa wingi katika kupima saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti  ili kusaidia kupunguza ongezeko la ugonjwa huo na kutakiwa kuwahi mapema kupima kabla ya tatizo kuwa kubwa kwani saratani inaweza kutibika kwa gharama nafuu kabisa.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, jinsia,wazee, na watoto Ummy Mwalimu na kusema kuwa vituo vya afya vihakikishe vinatenga siku maalum kila mwezi kwa lengo la wanawake kupatiwa huduma ya upimaji wa saratani ya matiti pamoja na shingo ya kizazi na huduma hizi zinatolewa bila malipo ili kuhamasisha upimaji kwa wanawake hapa nchini.
"Wanawake wajitokeze kwa wingi katika kupima ili kujua afya zao na hii itasaidia kupunguza saratani ya matiti  pamoja na shingo ya kizazi kwa kina mama,kuliko kusubiri tatizo liwe kubwa kwani tatizo likiwa dogo saratani inatibika na kwa gharama ndogo kabisa kuliko kukaa na kusubiri kuwa kubwa ". Amesema 
Amesema katika kuboresha huduma hizo serikali imenunua mashine za kisasa kabisa 100 za tiba mgando,mashine 9 za upasuaji mdogo ambazo zitatumika kwa ajili ya matibabu ya awali ya saratani kwa wanawake pamoja na mitungi 173 ya gesi ya carbon dioxide zitakazowezesha mashine hizo kufanya kazi.
Aidha Waziri  ametoa onyo kwa waganga wa kienyeji wanaowarubuni watu  kuwa wana uwezo wa kutibu ugonjwa huo kutokana na miti shamba  na kuwataka kuachana na hio tabia Mara moja kwani dawa za asili hazitibu saratani ila zinatuliza tu.
" Hakuna dawa ya tiba asili inayotibu saratani waganga wa kienyeji waache tabia ya  kuwarubuni wananchi kuwa dawa hizo zinatibu saratani jambo ambalo siyo kweli ila dawa hiyo inapunguza tuu maumivu na kama kuna mtu anaudhibitisho kuwa inatibu alete ifanyiwe uchunguzi ili tubaini kama ni kweli inatibu". Amesema.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndungulile amesema kuwa katika kupunguza gharama za matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje,Serikali ya awamu ya tano imeamua kuboresha huduma za afya hususani upande wa saratani ili kuweza kuhakikisha wagonjwa hao wanatibiwa hapa nchini.
"Ifahamike kuwa takribani wagonjwa wapya elfu 50 kila mwaka wanagundulika kuwa na saratani ,na idadi hii inakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2020".Amesema.
 Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii, jinsia,wazee, na watoto Ummy Mwalimu (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam juu ya Utaratibu wa utoaji wa matibabu ya Saratani bure kulia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine  Ndungulile  akifatilia kwa makini

Waziri  wa Afya Ummy  Mwalimu  pamoja na Naibu Waziri wa Afya Dkt Faustine Ndungulile wakipokea vifaa ivyo vilivyotolewa kwa lengo la kufanya upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi pamoja na matiti kwa wanawake nchini ambapo vifaa ivyo vitasambazwa katika vituo vya afya mbalimbali  vitakavyotoa huduma hizo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...