Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

KATIKA kuhakikisha Vifo vinavyotokana na uzazi kwa kina Mama vinapungua,Jamii imehimizwa kumpeleka mzazi kwenda kwenye vituo vya Afya ambavyo vina wataalamu ,kwani hatua hiyo ndio njia ya kusaidia kuondokana vifo hivyo.

Hayo yamebainishwa na Mratibu Taifa wa Muungano wa UtepeMweupe na Uzazi Salama, Rose Mlay wakati wa mkutano wa wadau wakati wa Mkutano wa Wadau wa Afya na Mama na Mtoto uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kupoteza mtoto na mama ni ajali ambayo inatokana na kukosekana kwa huduma sahihi wakati wa kujifungua.

Amesema kuwa mkutano wadau ni pamoja na kujadili takwimu za Afya ya Mama na Mtoto pamoja na kuweka mikakati ya kupunguza vifo vya uzazi.

Mlay amesema kwa sasa vifo vya wakina Mama vimeongezeka kutoka kwa vifo 24 vya wakinamama kwa siku hadi kufikia vifo 30 kwa siku huku akisema ongezeko hilo limechangiwa na wakina Mama kujifungulia sehemu zisizo salama,
Profesa Innocent Ngalinda Mtaalam Mshauri wa takwimu akitoa mada katika warsha ya kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi iliyoandaliwa na Taasisi ya Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for Safe Motherhood Tanzania (WRATZ)ambapo mambo mbalimbali yanajadiliwa na wadau kutoka taasisi mbalimbali hapa nchini ili kutatua changamoto zinazokabili huduma ya Mama na mtoto, Warsha hiyo inafanyika kwenye hoteli ya Regency Park Mikocheni jijini Dar es salaam
 
Bi. Rose Mlay Mratibu wa Taifa wa Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for Safe Motherhood Tanzania (WRATZ) akifafanua jambo wakati alipokuwa akitoa mada katika Warsha hiyo iliyojadili mambo mbalimbali yanayohusu kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua na salama kwa mama na mtoto nchini.
 
Kutoka kushoto ni Tausi Sued kutoka Taasisi ya Childbirth Survivas International ya Marekani, Angelina Ballat kutoka Taasisi ya Childbirth Survivas International, Julieth MawallaKutoka Halmashauri ya Wilaya Ubungo na Sara Luaimay kutoka Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni wakifuatilia mjadala huo.
Anna Sawaki Ofisa Mawasiliano na Habari Taasisi ya Utepe Mweupe White Ribbon Alliance for Safe Motherhood Tanzania (WRATZ) akifafanua jambo katika warsha hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...