Na mwandishi wetu, Kagera
Mkoa wa Kagera umeweka bayana nia yake ya kuchangamkia fursa za mikopo nafuu inayotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kuwasaidia katika kuendeleza shughuli za kilimo na uzalishaji mkoani humo.
Akizungumza wakati ugeni kutoka TADB ulipotembelea mkoani Kagera, Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu alisema Mkoa wake upo tayari kutumia fursa za mikopo nafuu inayotolewa na TADB ili kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara mkoani humo.
Aliongeza kuwa mkoa wa Kagera ipo tayari kutumia fursa za uwepo wa Benki ya Kilimo ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini mkoani humo.
Mkuu wa mkoa huyo alisema kwa kuzingatia malengo ya uanzishwaji wa Benki ya Kilimo unalenga kutimiza dhamira ya Serikali ya kuwasaidia wakulima nchini kote kukabiliana na mapungufu kwenye kuongeza tija katika shughuli zao za kilimo.
“Kwa kuzingatia majukumu ya kuanzishwa kwa Benki ya Kilimo, Mkoa wa Kagera upo tayari kufanya kazi bega kwa bega ili kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo mkoani kwetuu,” alisema.
Alitoa wito kwa wakulima wa mkoa wa Kagera kuchangamkia mikopo nafuu ya Benki ya Kilimo ili wajiongeze tija katika kilimo chao kwa kuwa Benki hiyo ipo kwa ajili ya kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika  kilimo nchini.
 Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu (katikati) akizungumza na ugeni kutoka Benki ya Kilimo ulipomtembelea Ofisini kwake Mkoani Kagera. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila na Katibu Tawala, Mkoa wa Kagera, Diwani Athumani (kulia).
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Kilimo, Bibi Rosebud Kurwijila (kushoto) akizungumza na Mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (Mstaafu) Salum Kijuu (katikati) na wakuu wa wilaya wa mkoa wa Kagera wakati walipotembelea mkoa huo. Kulia ni Katibu Tawala, Mkoa wa Kagera, Diwani Athumani.
 Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Bw. Dome Malosha (aliyesimama) akizungumza wakati walipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya ya Mkoa huo (hawapo pichani).
Ugeni kutoka Benki ya Kilimo wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Wakuu wa Wilaya na viongozi waandamizi wa Mkoa huo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...