Kaimu Mkurugenzi Mkuu (NIDA), Ndg Andrew W. Massawe amewasili mkoani Mara akiwa ameambatana na Kamishna Generali wa Idara ya Uhamiaji nchini Dkt. Anna Peter Makakala tayari kwa uzinduzi rasmi wa kuanza kwa zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Mkoa huo utakaofanywa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mhandisi Hamad Masauni.
Mara baada ya kuwasili viongozi hao walipokelewa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Malima ambaye aliwatambulisha kwa wananchi wa Bunda kabla ya kukutana na Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe.  Annarose Nyamubi  ambaye pamoja na kuwapa ripoti ya maandalizi ya Usajili kwenye Wiilaya yake, walipata fursa kutembelea Kambi ya JKT Butiama kukagua mafunzo kwa vijana ambao wataendesha zoezi hilo ndani ya siku 60.
Akizungumza na vijana katika Kambi hiyo, ndg. Masssawe amewataka kuwa wazalendo na makini katika zoezi wanalokwenda kulisimamia kwa kuhakikisha wanalifanya kwa uangalifu na nidhamu ya hali ya juu kwa faida ya Taifa lao.
“ tunafarijika sana tunapoona zoezi hili likiendeshwa na vijana wa JKT kwani mara zote wamekuwa wakijitoa kufanya kazi nzuri yenye uzalendo wa kweli kwa Taifa lao; ndiyo maana nawapongeza kwa dhati uongozi wa Mkoa na Wilaya kwa kuamua kusimamia zoezi hili na kuweka malengo ya utekelezaji, na sisi tunaahidi kwenu hatutawaangusha” alisisitiza.
Uzinduzi wa zoezi la Usajili kwa mkoa wa Mara utafanyika Jumapili 19/11/2017 na unategemewa kuhudhuriwa na viongozi wote wa Mkoa wakiwemo wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Madiwani, watendaji na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji, watumishi wa umma, Viongozi wa Dini na Wananchi. 
 Kamishna Generali wa Idara ya Uhamiaji nchini Dkt. Anna Peter Makakala, akizungumza jambo wakati alipowasili ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe. Annarose Nyamubi  (Aliyeketi Katikati). 
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu (NIDA) Ndg. Andrew W. Massawe akiweka saini kitabu cha wageni alipotembelea Kambi ya JKT Butiama kukagua mafunzo kwa vijana watakaoshiriki kuendesha zoezi la Usajili Vitambulisho vya Taifa.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu akipokea maelezo ya namna mafunzo yanavyotolewa kwa vijana wa JKT. Katikati ni Afisa wa Nida mtaalamu wa mifumo ya komputa Bw Godfrey Surera ambaye amekuwa akiendesha mafunzo hayo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Nida akisisitiza jambo mbele ya vijana wa JKT (Hawapo pichani) wakati alipotembelea kambi ya Butiama kukagua mafunzo ya namna ya kutumia mashine yanayoteolewa kwa vijana wa JKT. Kulia ni  Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe. Mhe.  Annarose Nyamubi 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...