30/12/1935                                                                                         
 22/11/2004

SABINUS        PETER    KWEKA
Baba yetu mpendwa, leo umetimiza mwaka wa 13 tangu ulipotwaliwa gafla na Bwana Picha yako uliyoipiga siku ya mwisho inatukumbusha uwepo wako tulipokuwa sote hapa duniani, na hasa upendo wako na wingi wa busara.

Ni vigumu kukubali kwamba haupo nasi lakini hatuna budi kuamini kwamba uko nasi kiroho kwa vile tunaye Mungu ambaye  anaendelea kututia nguvu kila iitwapo leo. Busara zako zinazidi kutuimarisha kila siku na tunaendelea kuzingatia maneno yako uliyokuwa ukihimiza juu ya kuwa na umoja katika familia na upendo kwa watu wote huku tukiendelea kumtumainia Mungu wetu ambaye amekuita kwake.

Unakumbukwa sana na sisi wanao tuliobaki, JANE,FESTO,EUGENIA,ELIZABETH,CECILIA NA THADEI, Dadako SR. DEVOTHA KWEKA  CDNK, WA – Narumu wote, ndugu, jamaa na marafiki kokote pale walipo.

Misa ya kumbukumbu imefanyika leo – Parokia ya Mkolani – Mwanza.
Tumaini letu linajengwa na neno lisemalo “Umevipiga vita vilivyo vizuri, Mwendo umeumaliza na imani umeilinda (2 Tim-4-7)”

Tunaomba  Eee Bwana Uendelee  kuipumzisha roho yake mahali pema peponi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...