Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa Shilingi Milioni 10 za Kitanzania kwa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart inayosimamia zoezi la kutokomeza kazi feki za sanaa nchini.

Kiasi hicho cha Pesa kimetolewa katika Kampuni hiyo ya Msama ili kuendesha vizuri mapambano dhidi ya wanaodurufu kazi hizo sehemu zote za jiji la Dar.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake, Mkurugenzi wa Msama Auction Mart, Alex Msama amesema kuwa Kampuni hiyo inamshukuru Mkuu huyo wa Mkoa kwa kufanya jambo kubwa na la mfano ambalo hakulitegemea.

"Sikutegemea kuona kama Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam anawapenda Wasanii, baada ya kuniita na kuniambia kuwa kazi ninayoifanya ya kupigania haki za Wasanii ni nzuri", amesema Msama."Ameniita amenimbia kazi inaenda vizuri, kwani amejaribu kupita maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar wala haoni Kompyuta, CD Feki na ameona kila CD anayoishika ina Stika ya TRA", ameongeza Msama

Aidha, Msama ameendelea kusisitiza kwa Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanafanya biashara yakuuza Kazi Feki za Sanaa waache kwa kutafuta kazi zakufanya.Pia amewaasa Wananchi kununua Filamu zenye Stika ya TRA inayong'aa vizuri, kwani watapofanya hivyo Wasanii hao watanufaika na kazi zao pamoja na kulipa Kodi kwa manufaa ya Taifa.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Auction Mart, Bw. Alex Msama akizungumza na Wanahabari mapema jana jijini Dar,akieleza taarifa ya Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam,Mh Paul Makonda kuongeza nguvu katika suala zima la kupambana na uharamia wa kazi sanaa hapa nchini,ambapo Mh Makonda amechangia milioni 10 kwa kampuni ya Msama Auction Mart ambayo inasimamia shughuli hizo za kupambana na Maharamia hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...