Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA akikagua gwaride ndani ya Meli hiyo mara baada ya kuwasili Bandari ya Dar es salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA akionyeshwa moja ya Helikopta zilizomo katika Meli hiyo mara baada ya kuwasili Bandari ya Dar es salaam.

………………………………………………………………………………

Meli kubwa ya Jeshi la Jamuhuri ya China yenye Hospital ndani imewasili Leo ikiwa na Madaktari Bingwa 381,Vifaa na Madawa ya kutosha kwaajili ya kuanza kwa zoezi la Upimaji na Matibabu Bure kwa wakazi wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA ametembelea Meli hiyo na kujionea namna imesheheni Vifaa tiba vya Kisasa ambapo ndani yake vipo vyumba 8 vya Upasuaji, Vyumba vya ICU, Wodi za Wagonjwa, Vyumba vya Madaktari, Mitambo ya kisasa, Mahabara na Sehemu ya Wagonjwa kupumzika.

Meli hiyo ya kipekee ina Helicopter kwaajili ya wagonjwa ambapo kwa Ulimwenguni Meli za Aina hiyo zipo Mbili pekee ambapo moja ni hii iliyokuja Tanzania na nyingine ipo Nchini Marekani.

RC MAKONDA amesema Meli hiyo ina mfumo maalumu wa Mawasiliano Kati ya Meli na Taifa la China pale inapotokea Ugonjwa umeshindikana.Tayari Jopo la wataalamu 30 wameenda Hospital za Amana, Temeke, Mwananyamala na Ocean Road kwaajili ya kukarabati na kufunga vifaa vipya kwa vile vitakavyobainika vilivyoharibika au Kufa.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Hakuna mwananchi anaepoteza maisha kwa kigezo cha kukosa huduma.Amewasihi Wananchi wenye magonjwa yaliyoshindikana kwa muda mrefu kuchangamkia Fursa hii ya matibabu Bure chini ya Madaktari Bingwa kutoka China.

Kwa upande wake kiongozi Mkuu wa Meli hiyo Kamanda GUAN BAILIN amesema wamekuja na vifaa vya kutosha na madaktari waliobobea hivyo wananchi Wajitokeze kwa wingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...