Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amewahamasisha wazee kuanzia
umri wa miaka 60 na kuendelea kujitokeza kwenye zoezi la upigwaji picha
ili waweze kupatiwa kadi za bima ya afya zitakazowawezesha kupatiwa
matibabu bure kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali.

Hayo ameyazungumza mara baada kuwasili katika Ofisi za Mtendaji Kata ya
Kabuku Nov 23, 2017 kuhamasisha huduma za afya.

Hatua hiyo ni muendelezo wa agizo la serikali ya awamu ya tano ya rais
Dkt. John Pombe Magufuli ya kuhakikisha wazee kuanzia umri wa miaka 60
na kuendelea wanapatiwa matibabu bure. PICHA ZOTE NA
KAJUNASON/MMG-KABUKU, HANDENI.

Wazee wakisikiliza kwa makini.
Diwani wa Kata ya Kabuku, Amina Mnegelo akizungumza machache mbele ya
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe huku wazee wakimfuatilia kwa
makini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...