Patrick Mvungi- MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) imeokoa zaidi ya shilingi Bilioni 5 ambazo zingetumika kusafirisha wagonjwa nje ya nchi kufuata matibabu baada ya MOI kuanzisha huduma za kibingwa ambazo awali zilikua hazipatikani hapa nchini.

Hayo yamebainishwa katika ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia Wazee na watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya alipotembelea MOI na kukagua hali ya utoaji wa huduma, mazingira , miundombinu na kuwajulia hali wagonjwa pamoja na kukutana na menejimenti.

Akizungumza na menejimenti ya MOI, Dkt. Ulisubisya amepongeza kazi nzuri na kubwa inayofanywa ambayo imepelekea watanzania kupata huduma bora za kibingwa ambazo wangepaswa kuzifuata nje ya nchi.

“Mnafanya kazi nzuri sana, jambo ambalo linatupa faraja kubwa sisi viongozi wenu, naomba muongeze ubunifu zaidi, hamtakiwi kuifikiria MOI kwenye ukanda huu wa Afrika pekee bali duniani, hii ni changamoto kwetu sote kuifikisha hapo ”alisisistiza Dkt. Ulisubisya

Aidha, Dkt Ulisubisya amesema MOI imepunguza rufaa za kwenda nje ya nchi kwa asilimia 95% na asilimia 5% iliyobaki MOI inaweza kuimaliza kabisa na kusiwepo mgonjwa wa kwenda nje ya nchi.

Pia, amewaelekeza viongozi wa MOI kushirikiana na Wizara ya Afya kutafuta namna ya kufuta rufaa kwa kutoa mapendekezo na ushauri utakaosaidia kutatuliwa kwa changamoto hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akizungumza na menejimenti ya MOI (hawapo pichani) katika ukumbi wa Mikutano wa MOI.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akimjulia hali mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji mkubwa wa mgongo, anayetoa ufafanuzi wa namna upasuaji huo ulivyofanyika ni Dkt. Nicephorus Rutabansibwa (Daktari bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Mgongo). Kushoto ni Mganga mkuu wa Serikali Profesa Muhamed Kambi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya akikagua mashine mojawapo katika benki ya damu ya MOI.
Mtaalamu wa Maabara Bwana Mbuta Jackson akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia , Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya kuhusu namna benki mpya ya damu inavyofanya kazi kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa damu salama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...