Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akizungumza wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya kushiriki mnada wa tano wa Korosho, Jana Novemba 17, 2017. Picha na Mathias Canal
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa akimuonyesha Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa jinsi magunia yalivyopangwa kwa ustadi ktika gala la kuhifadhia Korosho la Mtanda mara baada ya  Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya kushiriki mnada wa tano wa Korosho, Jana Novemba 17, 2017.
Badhi ya wakulima wa zao la korosho wa Chama cha Ushirika cha Masasi-Mtwara Cooperative Union Ltd (MAMCU) wakifatilia mnada wa tano wa korosho katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara. Jana Novemba 17, 2017.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Wa Tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wazee maarufu wa kijiji cha Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa (Wa Kwanza Kushoto), na Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini Mhe Hawa Ghasia (Wa Kwanza Kulia).
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza ushauri sambamba na pongezi kwa kushiriki Mnada wa tano wa Korosho Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara  wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Humo, Jana Novemba 17, 2017
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa wakikagua magunia ambayo tayari yamewasili katika Ofisi ya Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama Kikuu cha ushirika mara baada ya kumalizika kwa mnada wa tano wa Korosho Kijijini Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara.

Na Mathias Canal, Mtwara
NAIBU Waziri wa Kilimo Mhe Mary Machuche Mwanjelwa leo Novemba 18, 2017 amemuagiza Mrajisi wa vyama vya ushirika kukamilisha haraka kazi ya uchunguzi kwenye Bodi za vyama vya ushirika vya Mkoa wa Mtwara ili kubaini sababu zilizopelekea kuuzwa kwa magunia kiholela.

Alisema kuwa kumalizika kwa uchunguzi huo kutarahisisha kuchukuliwa haraka hatua kali za kisheri kwa wale wote watakaobainika kukiuka sheria No 17 ya vyama vya ushirika.

Naibu waziri alitoa agizo hilo wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Chiungutwa, Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mara baada ya kugundua kuwa kuna viashiria vya ukiukwaji wa taratibu katika upatikanaji wa magunia ya kuhifadhia korosho wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani humo.

Sambamba na hilo Naibu waziri Mhe Mwanjelwa wakati wote wa mkutano huo ameshuhudia malalamiko kutoka kwa wakulima wa zao la korosho wa Chama cha Ushirika cha Masasi-Mtwara Cooperative Union Ltd (MAMCU) kuhusu ucheleweshwaji wa upatikanaji wa maguni kutoka kwa mzabui, Mapungufu ya kilo kati ya PDA na WHRs ghala kuu, ikiwa ni pamoja na kuchelewa kwa malipo ya wakulima kwa njia ya benki kutoka kwa wanunuzi.

Katika ziara yake hiyo kilio cha wananchi wengi na wakulima walisiitiza zaidi kuhusu kukosekana kwa magunia hayo huku wakieleza kuwa wakati mwingine kuchelea kufika ama kutowafikia kabisa jambo ambalo linachangia kupunguza thamani ya zao la korosho.

“Nataka Mrajisi ufanye na ukamilishe kazi yako ya uchunguzi na baada ya kuipata taarifa hiyo hatua stahiki zitachukuliwa kwa wale wote watakaogundulika kukiuka sheria ya nchi” Amekaririwa Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa

Mbali na agizo hilo Naibu Waziri pamoja na wabunge wa Mkoa wa Mtwara walipata nafasi ya kujionea mnada wa tano wa ununuzi wa korosho unavyoendelea.

Hata hivyo Mnada wa tano ulishuhudiwa Kilogramu 7,524,104 za korosho zikiuzwa kwa thamani ya zaidi ya Bilioni 30.

Wakati huo huo Naibu Waziri Mhe Mwanjelwa amesema Wizara itayafanyia kazi haraka mapendekezo ya tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Gasper Byakanwa kufanya uchunguzi kuhusu mwenendo mzima wa magunia pamoja na upatikanaji wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...