Na Eliphace Marwa
BALOZI wa Oman Ali Al Mahruqi amesema Wafanyabiashara wa nchi hiyo wamevutiwa na na hatua mbalimbali znazochuliwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika kujenga mazingira bora kwa wawekezaji na wengi wao wapo mbioni kuja kuwekeza katika miradi mikubwa ya maendeleo nchini.

Balozi Al Mahruqi aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wa mazungumzo baina yake na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Kakunda na kuongeza kuwa suala la usalama wa mitaji yao ni jambo ambalo Wafanyabiashara hao wanapenda kuhakikishiwa na Serikali ya Tanzania.
Balozi Mahruqi alisema miongoni mwa fursa zinazowavutia Wafanyabiashara wa Oman kuja kuwekeza nchini ni pamoja na ubora wa miundombinu katika sekta za elimu na mifugo ikiwemo upatikanaji wa tasnia ya nyama.
“Serikali ya Oman ina mpango wa kuja kuwekeza katika ukanda wa Afrika Mashariki na kipaumbele kikubwa kitakuwa ni nchi ya Tanzania kutokana na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo Tanzania,” alisema   Balozi Mahruqi.
Aidha Balozi Mahruqi aliitaka Serikali kuharakisha makubaliano ya mikataba baina ya Mataifa hay ili kuwezesha wawekezaji kutoka Oman kupata fursa ya kuwekeza nchini na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji kutoka Oman.
Kwa upande wake Naye Naibu  Waziri Kakunda alimuahidi Balozi Mahruqi kufanyia kazi changamoto zilizopo ili kuhakikisha wawekezaji kutoka Oman wanakuja kwa wingi kuwekeza nchini bila ya kuwa na hofu ya usalama wa mitaji yao.
“Nitafuatilia kwa kina kwa wataalamu weu wanaohusika na uwekezaji kwenye kiwanda cha nyama ambapo wawekezaji kutoka Oman watawekeza takribani dola milioni tatu ambazo zitasaidia wafugaji wa Watanzania kupata soko la mifugo yao” alisema Naibu Waziri Kakunda.
Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL Mahruqi akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi ya Naibu Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (kushoto) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu wa Naibu Waziri huyo Bi. Debora Mkemwa.
Naibu Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda (katikati) akizungumza jambo alipotembelewa na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. AL Mahruqi leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais - TAMISEMI anayeshughulikia Afya Bibi. Zainabu Chaula.
 Naibu Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda akizungumza jambo na Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Ali A. AL Mahruqi walipokutana leo Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Oman nchini Tanzania Mhe. Ali A. AL Mahruqi akizungumza jambo na Naibu Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Joseph Kakunda alipomtembelea Ofisi kwake leo Jijini Dar es Salaam.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...