Na Lorietha Laurence- WHUSM, Arusha.
Serikali
imeahidi kushirikiana kwa ukaribu na wadau wa mchezo wa Golf nchini
katika kuhakikisha mchezo huo unafundishwa kuanzia ngazi ya chini ili
kuandaa wachezaji bora wa kimataifa wataoiwakilisha nchi katika
mashindano hayo duniani.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe alipokuwa akifunga mashindano ya Kili Golf Mkoani
Arusha ambapo ameeleza kuwa mchezo huo ni wa muhimu ukazingatiwa katika
kukuza sekta ya michezo.
“Mchezo
huu wa Golf ni mzuri sana kwa kuwa unakusanya watu wa tamaduni
mbalimbali na kuwaleta pamoja nami naahidi kuwa Wizara yangu
itahakikisha inashirikiana kwa karibu na wadau wa Golf nchini ili
kuukuza zaidi” amesema Mhe. Dkt. Mwakyembe.
Mhe.
Dkt. Mwakyembe ameongoza kwa kuwataka washiriki wa mchezo huo kuwa
mabalozi wazuri katika kuutangaza mchezo huo ndani na nje ya nchi na
kuhamasisha vijana wengine kuwa na moyo wa kujifunza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Katikati) akiwa amewasili katika Viwanja vya Kili Golf Jumapili Mkoani Arusha kwa ajili ya kufunga mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf Kulia ni Katibu Wake Bw. Andrew Magombana na kushoto ni Bw. Chris Martin Makamu wa Rais wa Umoja wa Golf Tanzania(Tanzania Golf Union).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (Kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kili Golf Bw. Bastiaan Bruins (Kushoto) baada ya kuwasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya kufunga mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf katikati ni Makamu wa Rais wa Umoja wa Golf Tanzania(Tanzania Golf Union) Bw. Chris Martin.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ( wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na waandaji wa mashindano ya Wazi ya Kili Golf Mkoani Arusha.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa risala kwa washiriki wa mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf katika halfa ya kufunga mashindano hayo jana Mkoani Arusha.
Mshiriki kutoka Kenya Bw. Edwin Mudanyi akijiandaa kupiga mpira wakati wa fainali wa mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf jana Mkoani Arusha ambapo jumla ya washiriki 250 kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Zambia, Afrika ya Kusini na Tanzania walishiriki.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimpa mkono wa hongera mmoja wa washindi wa kwanza Bw. Victor Joseph kutoka Tanzania baada ya kumalizika kwa mashindano ya Wazi ya Tanzania Kili Golf jana Mkoani Arusha.(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM).
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...