Na John Nditi, Morogoro

UONGOZI wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) umeingia makubaliano ya pamoja na Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne , Dk Jakaya Kikwete ili kulitumia shamba lake la mifugo lililipo kijijini kwake Msoga , liwe shamba darasa la kutolea elimu ya vitendo kwa wanafunzi wao , wataalamu wa mifugo na wafugaji.

Makamu Mkuu wa SUA , Profesa Raphael Chibunda alisema hayo Nov 20, 2017 wakati Rais Mstaafu Kikwete alipofanya ziara ya siku moja na wataalamu wake wa Mifugo walipofika Chuoni hapo kwa ajili ya kujifunza kuhusu ufugaji bora wa Ng’ombe wa maziwa.

Rais Mstaafu Kikwete kwa sasa amejikita zaidi kwenye suala la ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa maziwa , kilimo cha mazao ya chakula na matunda hasa mananasi kijijiji Msoga, Chalinze , wilayani Bagamoyo , mkoa wa Pwani.

“ Tumemwomba Rais Mstaafu Kikwete lile shamba lake la mifugo tulitumie kuwa ni shamba darasa kwa wanafunzi wetu wa Sanyansi ya wanyama , ukuzaji viumbe majini na Nyanda za Malisho pamoja na wataalamu wa mifugo na wananchi hasa wafugaji” alisema Profesa Chibunda na kuongeza .

“ Katika ombi letu naye ameridhia shamba hilo litumike kuwa shamba darasa” alisema Profesa Chibunda.Makamu mkuu wa Chuo hicho alisema , kwa kuridhia kwake , SUA inaweza kusongeza elimu bora ya ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa maziwa na nyama na matumizi ya malisho bora kwa wafugaji kutoka maeneo mbalimbali ya karibu na nje badala ya mtu mmoja mmoja kufika Chuoni hapo.

Kwa upande Rais Mstaafu alisema “ Nimefuata kujifunza na nimelizika na nilichokifuata na nimekipata na ahadi yangu kwenu SUA nitaendeela kushirikiana nayi , lengo ni kuleta mabadiliko ya kisayansi ya sekta ya ufugaji iweze kumletea tija mfugaji” alisema Rais Mstaafu Kikwete.

Naye Naibu makamu mkuu wa chuo hicho , Profesa Peter Gilla alisema, Sua itaendelea kufanya tafiti mbalimbali kwenye sekta ya Kilimo na Mifugo na kupanua wigo wa uzalishaji mkubwa wa mbegu za aina mbalimbali zikiwemo za matunda kwa nia ya kimaabara ya uhandisijeni ili kuwezesha mahitaji katika soko la Dunia. 
 Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Sayansi ya wanyama ,ukuzaji viumbe maji na nyanda za malisho , Dk Nazael Madalla  ( mwenye kuvaa miguuni  mabuti ya mvua ) kuhusu mashine ya kusaga majani ya malisho  ya mifugo hasa  ng’ombe wa maziwa ,wakati alipofanya ziara ya siku moja  ya kujifunza  ufugaji wa kisasa  katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Novemba 20, 2017  na ( watano kutoka kulia  ) ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Raphael Chibunda . 
 Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete, akiangalia  aina ya majani ya malisho yaliyosagwa na mashine kwa ajili ya kulisha   ng’ombe wa maziwa ,wakati alipofanya ziara ya siku moja  ya kujifunza  ufugaji wa kisasa  na malisho katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Novemba 20, 2017  na ( kushoto kwake ) ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Raphael Chibunda .

 Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete, akiwapatia ng’ ombe wa maziwa majani ya malisho yaliyosagwa na mashine  wakati alipofanya ziara ya siku moja ya kujifunza  ufugaji wa kisasa  katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Novemba 20, 2017 na ( kushoto  ) ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Raphael Chibunda .( Habari na Picha na John Nditi).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...