Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KIKOSI cha Yanga kimeendelea na mazoezi yake leo katika Uwanja wa Uhuru kujiandaa na mchezo wa raundi ya 11 ya ligi kuu Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons ya Jijini Mbeya.

Mchezo huo unatarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa Chamazi kutokana na mabadiliko yaliyofanya na bodi ya ligi baada ya Uwanja wa Uhuru kuwa na shughuli za kijamii.

Katika mazoezi hayo, mshambuliaji Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe aliyekosekana uwanjani kwa kipindi kirefu toka kuanza kwa ligi msimu huu leo amejumuika na wenzake na kufanya mazoezi kikamilifu kwa mara ya kwanza pamoja na wenzake ikiwa ni baada ya muda mrefu.

Kurejea kwa Tambwe katika mazoezi ya pamoja chini ya Kocha George Lwandamina  kuna uwezekano  kwenye mchezo wa wiki hii akajumuishwa kwenye mchezo dhidi ya TZ Prisons siku ya Jumamosi.

Kocha wa Yanga, Mzambia George ‘ Lwandamina amesema kwamba kati ya majeruhi wake wanne, wengine ni Tambwe pekee amefanya mazoezi ukiachilia  kiungo Thabani Kamusoko na mshambuliaji, Donald Ngoma nna kiungo Papy Kabamba "Tshishimbi" ambapo alikosa mchezo wa wiki iliyopita dhidi ya Mbeya City.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...