Na: Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari ya MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas  amesema Maafisa Habari na Mawasiliano hapa nchini wanatakiwa kuwa na uelewa wa masuala mbalimbali ikiwemo Uchumi, siasa na jamii katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Dkt. Abbas ameyasema hayo leo, Mjini Dodoma alipokuwa akifungua mafunzo ya Itifaki na Mawasiliano ya Kimkakati kwa Maafisa Habari na Mawasiliano kutoka Taasisi za Umma na Sekta Binafsi yaliyoandaliwa na Idara ya Habari MAELEZO kwa kushirikiana na Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) na  Washauri wa Kidiplomasia wa Kiuchumi (Economic Diplomacy Consultants).

 "Itifaki ni moja ya eneo ambalo Afisa Habari yoyote anatakiwa kulijua kwa undani kutokana na jukumu alilonalo la kusimamia matukio mbalimbali yanayotokea katika Taasisi yake," alisema Dkt. Abbas.

Ameendelea kwa kusema, kuna kipindi Afisa Habari anapata wageni ambao ni wakuu wa nchi na kushindwa kujua namna ya viongozi hao wanavyotakiwa kukaa kutokana na vyeo vyao.Aidha, amesema kuwa mafunzo hayo ni muendelezo wa mafunzo mengine mengi ambayo Maafisa hao watakuwa wakiyapata kila wakati ili kuwapa uelewa katika maeneo mbalimbali ya masuala ya uchumi, siasa, jamii na katika sekta yenyewe ya mawasiliano.     

"Itafika kipindi tutajifunza hata vyeo vya jeshi namna vinavyokuwa pamoja na majina ya vyeo vyao ambapo itarahisisha katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Maafisa Habari," alisema Dkt. Abbas.
Mafunzo hayo ya Maafisa Habari na Mawasiliano  ni ya siku mbili ambayo yameanza leo Novemba 23 na yanatarajia kumalizika kesho Novemba 24, 2017.
 Mkurugenzi  Idara ya Habari Maelezo na Msemaji  Mkuu  wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akifungua mafunzo kuhusu Mawasiliano ya Kimkakati na Itifaki  kwa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali na Sekta Binafsi  (hawapo pichani) yanayofanyika kwa siku mbili  mjini Dodoma.
Mkurugenzi  Idara ya Habari Maelezo na Msemaji  Mkuu  wa Serikali Dkt. Hassan Abbas akiongea na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali na Sekta Binafsi wakati ufunguzi wa mafunzo yanayofanyika kwa siku mbili  mjini Dodoma.(Picha zote na Frank Mvungi- Maelezo Dodoma)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...