NA VICTOR MASANGU, LUGOBA BAGAMOYO

KATIKA kukabiliana na wimbi la umasikini na ukosefu wa ajira kwa vijana pamoja na wanawake hatimaye halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani imeamua kuvipatia mikopo wa kiasi cha shilingi milioni 120 Vikundi 40 vya wajasiriamali kutoka kata 15 kwa lengo la kuweza kujikwamua kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi.

Akizungumza katika halfa ya makabidhiano ya hundi kwa ajili ya fedha hizo iliyofanyika katika kata ya Lugoba Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga ambaye alikuwa mgeni rasmi amesema lengo la serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufui ni kuhakikisha inawawezesha kiuchumi wananchi wake pamoja na kuwapatia mikopo ya fedha kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za ujasiriamali.

Aidha Mwanga aliwaagiza watendaji na viongozi kuhakikisha wanafuatilia kwa ukaribu vikundi vyote ambavyo vimeshakopeshwa kufanya ukaguzi wa kina kujua fedha amabzo zimetolewa zinatumika katika matumizi sahihi kwani amebaini kuna baadhi yao wanakwenda kinyume na taratibu zilizowekwa hivyo kurudisha nyuma kasi ya maendeleo.

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze Mohamed Sume akisoma taarifa yake amebainisha kuwa fedha hizo zote zimetokana na makusanyo yatokanayo na mapato ya ndani kwa lengo la kuweza kuviwezesha vikundi hivyo ikiwa ni kutekeleza Agizo la ya Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli ya kutenga asilimia kumi kwa ajili ya kuwawezesha vijana pamoja na wanawake.

Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Said Zikatimu amesema kuwa fedha ambazo zimetolewa katika vikundi vya wajasiriamali hao ni katika kota ya kwanza ambapo pia wametenga milioni 300 kwa lengo la kuweza kuvipatia vikundi vingine ili kuweza kuongeza pato la Taifa kupitia biashara wanazozifanya.

Alisema kwamba mipango ya halmashauri hiyo ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2020 vikundi vyote vya ujasiriamali vinawezeshwa kwa kupatiwa mikopo ya kufanyia biashara zao mbali mbali sambamba na kuwapatiua wataalamu ambao watakuwa wakiwafundisha namna na kuweza kujifunza masuala mbali mbali yanayohusina na namna na kuweza kutafuta masoko katika bidhaa wanazozizalisha.

Baadhi ya wajasiriamali ambao wamenufaika na fedha hizo akiwemo Zawadi Rashid pamoja na Mwajuma Shaban walieleza malengo na matarajio yao ni kuhakikisha wanakuza mitaji yao kwa kuendeleza biashara walizonazo, ikiwemo ufugaji, kilimo, ufyatuaji wa matofali pamoja na ujenzi wa viwanda vidogo vidogo ili kuweza kujikwamua kimaisha na kukuza uchumi.
 Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga akizungumza na vikundi mbali mbali vya wajasiriamali  havipo pichani  kutoka halmashauri ya Chalinze katika halfa fupi ya  makabidhiano ya hundi yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 120 ambayo itaweza kuwasaidia katika kufanya biashara zao.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze Said Zikatimu akizungumza jambo na vikundi vya wajasiriamali ambao walifika katika sherehe hiyo ya makabidhiano ambayo ilifanyika katika viwanja vya sokoni Lugoba.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Majid Mwanga kulia akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 120  mmoja wa wanakikundi wajasiriamali katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya soko la Lugoba(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...