WATUMISHI wa kada mbalimbali katika sekta ya afya bado wanahitajika nchini ili kuboresha huduma ya afya kwa ajili ya kuokoa maisha ya watanzania ili kuifikisha nchi katika uchumi wa viwanda mpaka kufikia 2020.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati wa mahafali ya pili ya chuo cha Afya na tiba cha KAM yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.

“Tuna malengo ya kuwa na watumishi wa kada mbalimbali za sekta ya afya wapatao laki 1.849 na kati ya hao tumefanikiwa kuajiri watumishi 89842 na bado tunahitaji watumishi 95800 ili kuweza kuwa na rasilimali watu” alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa wanakishukuru chuo hiko kwani wamekuwa na mchango mkubwa kwa kutoa rasilimali watu katika sekta ya afya kwani wametoa wataalamu wa afya wapatao 1600 mpaka hivi sasa.

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto Serikali kupitia Wizara ya afya imetoa shilingi milioni 700 kwa vituo vya afya ili kuweza kuboresha huduma za afya nchini.

“Tumetoa milioni 700 kwa kwa vituo vya afya vipatavyo 100 hapa nchini ikiwa milioni 400 kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya upasuaji na vyumba vya kujifungulia na milioni 300 ni kwa ajli ya kununua vifaa tiba” alisema dkt. Ndugulile.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akigawa vyeti kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Afya na Tiba KAM waliofanya vizuri kwenye masomo ya fani mbalimbali ya afya wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akigawa vyeti kwa baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Afya na Tiba KAM waliofanya vizuri kwenye masomo ya fani mbalimbali ya afya wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kushoto akipokea na zawadio kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo na tiba wa Chuo cha Afya na Tiba KAM dkt. Aloyce Musika kulia wakati wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Baadhi Wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile hayupo pichani wakati wa wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wahitimu wa kada mbali mbali za sekta ya afya wa chuo cha KAM wakimsikiliza wakati wa mahafali ya pili ya chuo chuo hiko yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.Picha Na Ally Daud- Wizara ya Afya (WAMJW).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...