Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa (Mb) anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu katika Mkoa wa Ruvuma kuanzia tarehe 23 - 25 Novemba, 2017.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 22 Novemba 2017 na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema Mheshimiwa Waziri Mkuu atawasili mjini Songea siku ya Alhamisi tarehe 23 Novemba, 2017 na kupokelewa na viongozi wa Chama na Serikali katika Uwanja wa ndege Songea majira ya 7.00 mchana.

Baada ya kuwasili atapokea taarifa ya maendeleo ya Mkoa na ile ya Chama Tawala Uwanja wa Ndege Songea. Kisha ataelekea Wilaya ya Namtumbo ambapo atafungua ghala la MIVARF, kuongea na Madiwani na watumishi wa Umma na baadaye ataongea na wananchi wa Namtumbo kwenye mkutano wa hadhara. Ijumaa tarehe 24 Novemba, 2017 Mheshimiwa Waziri Mkuu ataendelea na ziara yake kwa kuongea na wananchi wa kijiji cha Mchomoro kisha ataelekea Wilaya ya Tunduru ambapo atasalimia na wananchi wa vijiji vya Rahaleo,Milonde na Matemanga akiwa njiani kuelekea mjini Tunduru.

Aidha, Mheshimiwa Waziri Mkuu atatembelea kituo cha Afya cha Nakayaya, ghala la kuhifadhia Korosho na kupata taarifa ya Chama Kikuu Cha Ushirika TAMCU. Jioni Mheshimiwa Waziri Mkuu ataongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika mjini Tunduru katika uwanja wa michezo. Jumamosi tarehe 25 Novemba, 2017 Mheshimiwa Waziri Mkuu atahitimisha ziara yake mkoani Ruvuma na kurejea Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa Mndeme ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi katika mapokezi kuanzia uwanja wa Ndege Songea atakapowasili Aidha amewaomba wananchi kujitokeza kwenye maeneo yote ambayo Waziri Mkuu atapita na kwenye mikutano ya hadhara ili wapate fursa nzuri ya kumsikiliza Mheshimiwa Waziri Mkuu na kupokea maelekezo atakayoyatoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...