Huzuni, Majonzi pamoja na simanzi ilitanda ndani ya Nyuso za Wananchi wa Visiwa vya Zanzibar wakati ndege iliyochukuwa Miili ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ ) waliouawa Nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ilipotua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume.


Miili ya Wanajeshi hao ililetwa Nchini Tanzania juzi kwa ndege Maalum ya Umoja wa Mataifa ikitokea DRC na kupelekwa moja kwa moja Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania yaliyopo Lugalo Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kuiaga rasmi Kijeshi.



Ndege iliyowachukuwa Mashujaa hao wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ya JW 8029 iliteremsha Miili ya Askari Nassor Daudi Ali, Issa Mussa Juma, Hassan Abdulla Makame na Hamad Mzee Kamna.

Wengine kati ya askari hao Tisa ambapo Mmoja anapelekwa Kisiwani Pemba ni Ali Haji Ussi, Iddi Abdulla Ali, Juma Mossi Ali, Mwinchum Vuai Mohamed na Hamadi Haji Bakari.

Akitoa salamu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema kuuawa kwa Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} katika shambulio lililofanywa na Waasi wa ADF Nchini DRC ni la Kinyama lilikiuka misingi ya Haki za Binaadamu ambalo pia ni kinyume na makubaliano ya Ulinzi wa Amani wa Kimataifa.


Miili ya Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} ikiteremshwa kwenye ndege ya JW 8029 katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume ikitokea Mjini Dar es salaam.
Balozi Seif pamoja na Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu Meja General Sharif Sheikh Othman wakitoa heshima wakati Miili ya mwashujaa ikiteremshwa kwenye ndege.
Balozi wa Kuweit Nchini Tanzania Bwana Jassem Alnajem wa kwanza kutoka kushoto akijumuika pamoja na Viongozi wa Kiserikali katika kuipokea Miili ya askari wa Tanzania waliouawa Nchini DRC Wiki iliyopita.
Mawaziri mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakishuhudia kuwasili kwa Miili yaWanajeshi wa Tanzania waliouawa na waasi wa ADF Nchini DRC.
Balozi Seif akiongoza Viongozi na Wananchi wa Zanzibar katika kuipokea miili ya Makeshi ya Tanzania yaliyouawa Nchini Jamuhuri ya Kisemokrasi ya Congo.
Majeshi ya Wananchi wa Tanzania wakiichukuwa Miili ya Askari wenzao wakiwasili katika Viwanja vya Makao Makuu ya Brigedia Nyuki Migombani kwa ajili ya kuagwa rasmi Kiserikali.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu za pole kwenye shughuli Maalum ya Kuiaga Miili ya Wanajeshi wa JWTZ hapo Migombani Mjini Zanzibar.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...