Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii jioni ya leo inaeleza kuwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel  Nkaya Bendera,  amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili  jijini Dar es salaam alikokuwa amepelekwa kwa matibabu. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano hospitalini hapo Bw. Aminiel Eligaisha amethibitisha kifo cha Marehemu Bendera ambaye alisema alifikishwa hospitalini hapo Saa 6:30 mchana akitokea Bagamoyo na kupelekwa moja kwa moja katika wodi ya magonjwa ya dharura na kwamba ilipofika saa 10:24 jioni alifariki dunia. 
Marehemu amewahi kuwa Mbunge wa Korogwe mjini, Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kabla mauti hayajamkuta alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara kabla ya kustaafu kwa mujibu wa sheria hivi karibuni.
Marehemu Bendera atakumbukwa pia kama mmoja wa makocha wa timu ya Taifa ya soka ya Taifa Stars mwenye mafanikio makubwa kuliko makocha wote nchini, hasa kwa rekodi yake ya kuiwezesha Tanzania kushiriki kwa mara ya kwanza - na ya mwisho - kwenye michuano ya kombe la Afrika iliyofanyika nchini Nigeria mwaka 1980.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, akiemuelezea kama mtu aliyekuwa kiongozi shupavu, mahiri na mchapakazi aliyependa kufanya kazi kwa ushirikiano na kwamba daima akitamani kupata mafanikio katika majukumu yake yote.
Mola na aiweke Roho ya marehemu 
Bendera mahala pema peponi,
AMINA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...