Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ameendelea na ziara ya kukagua hatua iliyofikiwa katika ukamilishaji wa ujenzi wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme pamoja na njia ya kusafirisha umeme kutoka Makambako hadi Songea.

Lengo la ziara hiyo ni kukagua uimara wa mitambo ili Serikali kupitia TANESCO iweze kujipanga vizuri kwa kuwa na umeme wa uhakika.
Waziri wa Nishati Dkt MEDARD KALEMANI akiwa kwenye ziara ya Kukagua hatua iliyofikiwa katika ukamilishaji wa ujenzi wa vituo vya kupoza na kusambaza umeme pamoja na njia ya kusafirisha umeme kutoka Makambako hadi Songea.

"Kama ilivyo azma ya Serikali ya Awamu ya Tano kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda, tunahitaji kuwa na umeme wa uhakika". Alisema Dkt. Kalemani. Habari Wakuu naomba Mpokee Codes kwa ajili ya Kuhabarisha Umma.....Natanguliza Shukrani Katika ziara hiyo pia amekagua miradi ya umeme Vijijini Awamu ya Tatu inayoendelea katika Mikoa hiyo ili kuhakikisha inakamilika kwa wakati. Akikagua mradi wa kusafirisha umeme wa msongo wa kilovolti 220 kutoka Makambako hadi Songea, Dkt. Kalemani alisema mradi huo utaiunganisha Mkoa wa Ruvuma katika Gridi ya Taifa. Pia, kukamilika kwa miradi hiyo kutaipunguzia gharama Serikali kwa kuondokana na mitambo ya mafuta.
Pichani ni Baadhi ya vituo vya kupoza na kusambaza umeme pamoja na njia ya kusafirisha umeme kutoka Makambako hadi Songea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...